Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TBA yakabiliwa na uhaba wa watumishi, vifaa
Habari Mchanganyiko

TBA yakabiliwa na uhaba wa watumishi, vifaa

Spread the love

 

PAMOJA na Wakala wa Majengo Tanzania TBA kuweza kufanya kazi kwa mafanikio makubwa lakini bado inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa watumishi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TBA, Mhandisi Daudi Kangoro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa habari Maelezo juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika wakala huo.

Amesema kuwa Wakala kwa sasa wanauhitaji wa watumishi 811 ambapo kwa sasa wana watumishi 350 ikiwa ni sawa na upungufu wa watumishi 461 jambo ambalo linawalazimu kuajiri watumishi wa muda mfupi.

Pamoja na kuwepo na changamoto hiyo bado wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa vifaa ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa mtambo wa kuzalisha kokoto jambo ambalo linawapelekea kununua kokoto kwa bei ya soko.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kangoro amesema kuwa katika utekelezaji wa miradi ya TBA kwa kipindi cha kwanza 2021/22 hadi 2022/2023 jumla ya Sh 54.2 bilioni zimetumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa nyumba za watumishi 3,500 zinazojengwa eneo la Nzuguni katika jiji la Dodoma.

Aidha amesema wakala huo umeendelea kujenga nyumba za watumishi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za majaji sambamba na ujenzi wa nyumba za viongozi wastaafu zikiwamo za marais

Aidha Mhandisi Kangoro amesema kuwa Wakala huo unatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba kwa kiwango cha juu ambapo nia kubwa ni kutaka watumishi waishi maisha ya kuwawezesha kumiliki nyumba kwa bei nafuu.

Akizungumzia juu ya ujenzi wa nyumba za Nzuguni ameeleza kuwa nyumba zaidi ya 150 zimekamilika kwa asilimia 80 na zinatarajiwa kuanza kutumiwa mwisho wa mwezi Julai mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!