Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Nikki Haley ajitosa kumvaa Trump urais Marekani
Kimataifa

Nikki Haley ajitosa kumvaa Trump urais Marekani

Spread the love

GAVANA wa zamani wa jimbo la South Carolina, Nikki Haley amesema kwamba atawania uteuzi wa mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republikan.

Uamuzi huo unamfanya Haley kukabiliana na bosi wake wa zamani rais Donald Trump, ambaye alimteua kuwa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Haley mwenye umri wa miaka 51, alitangaza kupitia mitandao ya kijamii akisema rekodi ya rais Joe Biden hairidhishi na kwamba sasa wasaa wa kiongozi wa kizazi kipya.

Katika video hiyo ya zaidi ya dakika tatu, haikumtaja kabisa rais mstaafu Trump, ambaye mwezi Novemba alitangaza kuwa pia atawania uteuzi wa chama cha Republikan kugombea tena urais ambao alishindwa na Rais Joe Biden katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Katika video hiyo ameelezea miaka ya mwanzo akiwa South Carolina kama binti wa mhamiaji mhindi, ambaye alifanikiwa kuwa gavana kuanzia mwaka 2011 mpaka 2017 na kupewa wadhifa wa ubalozi wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017 mpaka 2018.

Uchaguzi mkuu ujao wa Marekani unatarajiwa kufanyika tarehe 5 Novemba 2024.

1 Comment

  • KAMA BADO ANA AMINI UTI WA MGONGO NI ELIMU KWENYE LIKE JICHO TUWEKE LIKE FATHER LIKE SON (HASA KWENYE KIFO CHAO) MAANA NILILIDHI NGOMBE NA UJUZI WA KUCHUNGA NGOMBE KUTOKA KWA BABU

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!