Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Babu Duni: Tutatumia mikutano ya hadhara kuikosoa Serikali sio kutukana
Habari za Siasa

Babu Duni: Tutatumia mikutano ya hadhara kuikosoa Serikali sio kutukana

Juma Duni Haji
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Juma Duni Haji amesema chama chake kitaitumia mikutano yahadhara kuisema Serikali kuhusu yale wanayopaswa kuyafanya kwa wananchi na sio kutukana. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mwenyekiti huyo ameyasema hayo leo  Jumapili ya tarehe 29 Januari 2023 katika Jimbo la kichama la Tumbe ambapo uongozi wote umekutana chini ya uongozi wa Katibu wa Mkoa wa Maweni kuzungumzia ujengaji wa chama.

Mkutano huo pia umelenga kuweka wanachama imara ,vilevile  kufanikisha mkutano wa hadhara utaofanyika tarehe 4 Machi 2023.

Juma Duni amesema tangu kuasisiwa kwa Mapinduzi ya Zanzibar 1964 hadi sasa bado wananchi wa Zanzibar hawajawahi kufaidi matunda yao,

“Maisha bado ni magumu sana kila awamu hali ndio ile ile,” amesema Juma Duni.

Amesema wakati wanaingia kwenye Serikali ya Umoja wa kitaifa walikubaliana kuundwa tume kufanya tathmini juu ya waathirika wa uchaguzi mkuu 2020 lakini hadi sasa haijaundwa tume hiyo “na Bwana mkubwa (Rais) hataki kabisa kuhusu hili.”

“Cha ajabu na chenye kushangaza siku Rais anakabidhiwa ripoti ya kikosi kazi hata haijafika ofisini kwake tukamuona anamteua Faina kuwa Mkurugenzi wa uchaguzi mtu ambae anapaswa kuwa miongoni mwa watu waliostahiki kuwa mahakamani hivi sasa,” amesema.

Pia Juma Duni amehoji sababu ya kutotolewa kwa ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa na Rais wa Zanzibar licha yakwamba kimeshamaliza kazi yake na kukabidhi ripoti kwa Rais.

“Rais Samia aliunda kikosi kazi na wakaja na ripoti lakini haikutosha mapendekezo ya ripoti hiyo yamewekwa hadharani,lakini chakushangaza Zanzibar hadi leo ripoti ya kikosi kazi imekaliwa kitako huku hakuna anaejua hatma ya ripoti hiyo,” amesema.

Katika hatua nyingine Juma Duni amesema suala la katiba mpya linapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa kwa sababu wahusika pande zote mbili hawakuungana bali wameunganishwa, “na kwa mshangao wahusika wa pande zote mbili hawaridhii muungano ulivyo sasa.”

Mbali na hayo amesema chama hicho kimepanga kwenda kuwaeleza Jumuiya za Kimataifa kuhusu uhalisia wa SUK na kwamba chama tawala hakioneshi dhamaira njema.

“Jumuia nyingi za kimataifa zilipata moyo na kuamua kurudi Zanzibar kwa sababu ya kuwaeleza tunaona mwanga kwenye muundo wa Serikali (GNU) lakini sasa tutarudi kuwaeleza uhalisia ulivyo wenzetu hawaoneshi dhamira njema.

“Tunataka maridhiano kwa sababu tumechoka kuteswa na hata kuuliwa watu wetu kwenye kila uchaguzi na ndio maana tunasimama kutaka mabadiliko na yenye  dhamira njema,” amesema Juma Duni

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya Uongozi Chama cha ACT-Wazalendo, Ismail Jussa, amewataka wananchi kujiandaa na kuonesha chama hicho kipo imara kuelekea mkutano wa hadhara utakaofanyika Nungwi Mkoa wa Kusini Unguja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!