Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Asilimia 86 wenye umri zaidi ya miaka 18 wapata dozi kamili ya Uviko-19
Afya

Asilimia 86 wenye umri zaidi ya miaka 18 wapata dozi kamili ya Uviko-19

Spread the love

 

KWA kipindi cha miezi sita kuanzia mwezi Julai hadi Desemba 2022 Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya wamefanikisha utoaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 na kufikia asilimia 86 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kupata dozi kamili ya chanjo dhidi ugonjwa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo tarehe 19 Januari, 2023 alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Afya kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2022 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Jijini Dodoma.

“Ndani ya miezi sita tumefanya vizuri kwenye utoaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19, tumefikia asilimia 86 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea kupata dozi kamili ya chanjo dhidi ya UVIKO-19 ukilinganisha asilimia 24.7 hadi kufikia mwezi Juni, 2022” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Amesema hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2022 jumla ya dozi 46,848,520 zilikuwa zimepokelewa ambapo dozi 41,581,670 zilikuwa zimesambazwa nchi nzima huku kiasi cha chanjo zilizosalia kwenye bohari ya kutunzia chanjo ni 5,266,850 ambazo zote ni aina ya J.J.

Amebainisha kuwa Wizara ya Afya hivi karibuni itazindua ‘Booster’ dozi ya UVIKO-19 ili wananchi waweze kuongeza kinga zaidi dhidi ya ugonjwa huo na kusema kuwa ni hiari kwa mtu yeyote kwenda kupata chanjo hiyo.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu

Kuhusu huduma za chanjo kwa Watoto, Waziri Ummy amesema huduma hizo ziliendelea kutolewa kwa Watoto wa chini ya umri wa mwaka mmoja kwa chanjo ya Penta3 ambayo hutumika kama kipimo kikuu ilifikia asilimia 107 ukilinganisha na mwaka 2021 iliyofikiwa kwa asilimia 96” amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema Wizara ya Afya imefanikisha vyema Kampeni ya utoaji wa chanjo ya Polio ya matone OPV3 katika raundi zote nne kwa asilimia 103 ukilinganisha na asilimia 79 mwaka 2021, sindano (IPV) kwa asilimia 107 ikilinganishwa na asilimia 95 kwa mwaka 2021, Surua rubella dozi ya kwanza asilimia 109 ikilinganishwa na asilimia 92 kwa mwaka 2021, Surua Rubella dozi ya pili asilimia 96 ilinganishwa na asilimia 76 kwa mwaka 2021.

“Kwenye utoaji wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana dozi ya kwanza (HPV1) tulifanikisha utoaji wa chanjo hiyo kwa asilimia 83 ikilinganisha asilimia78 kwa mwaka 2021 na chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana dozi ya pili (HPV2) asilimia 62 ukilinganisha na asilimia 61 kwa mwaka 2021” amesema Waziri Ummy Mwalimu kwenye taarifa aliyowasilisha kwa Kamati.

Waziri Ummy amesema kuwa Wizara imeendelea kuboresha huduma za afya mipakani na kuhakikisha kuwa magonjwa ambukizi yaliyopo katika nchi jirani hayaingii nchini.

“Tumefanya kazi kubwa ya usimamizi wa masuala ya afya mipakani kuhakikisha ugonjwa wa Ebola hauingii nchini, na habari njema tumesikia hivi karibuni nchi ya Uganda imetangaza kumaliza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kwa hiyo na sisi tunaamini tupo salama” amesema Waziri Ummy.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Stanslaus Nyongo ameipongeza Wizara ya Afya pamoja na Taasisi zake kwa kuendelea kusimamia vyema Sera ya Afya na kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za Afya.

Nyongo ameishauri Wizara ya Afya kushirikiana vyema na Ofisi ya Rais Tawala za Mikao na Serikali za Mitaa kufanya kazi kwa ushirikiano na kuhakikisha kuna usimamizi imara katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!