Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini
Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Mohammed Banda
Spread the love

 

MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida Big Star (U17), Mohammed Banda leo tarehe 19 Januari, 2023 amefariki dunia baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Singida … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Klabu hiyo kupitia akaunti yao ya mtandao wa Instagram, Banda alipoteza maisha alipofikishwa Hospitali ya Mkoa wa Singida baada ya kugongana kichwani na mchezaji mwenzake wakiwa mazoezini katika Uwanja wa Magereza, Singida.

“Tunathibitisha kutokea kwa kifo cha aliyekuwa mchezaji na kapteni wa timu yetu ya vijana (U17), Mohammed Banda, kilichotokea leo asubuhi Januari 19, 2023.

“Tunatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu mzito,” imesema taarifa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

GGML yaongeza udhamini kwa Geita Gold FC msimu wa 2022/2023

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeongeza mkataba wa...

error: Content is protected !!