Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Biteko: Ushirikiano kati ya Tanzania, Canada umeimarisha sekta ya madini
Habari Mchanganyiko

Biteko: Ushirikiano kati ya Tanzania, Canada umeimarisha sekta ya madini

Spread the love

 

WAZIRI wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Canada katika sekta ya madini umeendelea kuimarika hususan katika masuala ya utafiti wa madini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Biteko ameyabainisha hayo leo 19 Januari, 2023 mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Kyle Nunas Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma.

Dk. Biteko amesema baadhi ya maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa madini nchini Tanzania yaligunduliwa na kampuni za utafiti kutoka nchini Canada hivyo, upo ushirikiano mkubwa kwenye sekta ya madini kati ya nchi hizo mbili.

Aidha, Dk. Biteko amemweleza Balozi Nunas kuhusu mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 yaliyofanyika Mwaka 2017 likiwemo suala la ufungaji wa migodi, mazingira, na miongozo ya upatikanaji wa leseni za utafiti, leseni za uchimbaji mdogo, wa kati na mkubwa.

Pia, Dk. Biteko amesema Sheria ya Madini inazitaka kampuni zote za utafiti nchini kutoa taarifa za utafiti kila baada ya miezi mitatu ambapo kushindwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Pamoja na mambo mengine, Dk. Biteko ametoa wito kwa kampuni kutoka Canada kuwekeza Tanzania hususan katika sekta ya Madini ambapo amesema Kanuni na Miongozo mbalimbali katika sekta ya Madini inamlinda mwekezaji ili anufaike na watanzania wanufaike na uwekezaji huo.

Pia, Dk. Biteko amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na madini mbalimbali yakiwemo madini ya kimkakati yanayohitajika zaidi kwenye matumizi ya teknolojia za kisasa ikiwemo magari yanayotumia nishati ya umeme.

Mazungumzo hayo pia yamemuhusisha Naibu Waziri wa Madini Dk. Steven Kiruswa, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!