Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe: Chadema haitafuti vyeo mazungumzo na Samia
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Chadema haitafuti vyeo mazungumzo na Samia

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema mazungumzo ambayo chama hicho inafanya na Serikali ni ya wazi na wala hawatafuti vyeo au nafasi katika serikali zaidi ya mabadiliko ya kimfumo yatakayohakikisha demokrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu na fursa kwa wananchi kuboresha maisha yao.

Pia ameziomba Jumuiya za kimataifa kuendelea kupaza sauti kuhusu siasa za Tanzania, ili kulinda misingi ya demokrasia ya vyama vingi, utawala wa sheria na haki za binadamu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 10 Disemba, 2022 katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje wa Chadema kuhusu hotuba ya Mbowe katika Mkutano wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani (IDU), tarehe 9 Desemba 2022.

Mbowe alisema kwa sasa anaongoza Chadema katika mazungumzo na serikali kuponya majeraha na kurudisha demokrasia na kuwa msimamo wa Chadema katika mazungumzo hayo umekuwa wazi.

Alisema, jumuiya hizo ikiwemo IDU zina nguvu ndiyo maana hata alipokuwa rumande akikabiliwa na mashtaka ya ugaidi katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi, jijini Dar es Salaam, zilipaza sauti hadi akaachwa huru.

“Nipo huru leo na nashiriki kikao hiki mwenyewe kwa sababu IDU na wadau wengine wa kimataifa mlipaza sauti na kutaka niachiliwe huru kutoka gerezani bila masharti, kama msingefanya hivyo, ningekuwa nimeshasokomezwa gerezani maisha kutokana na mashitaka ya uongo niliyofunguliwa yasiyokuwa na dhamana,”

“Rai yangu siku ya leo ni ndogo tu, IDU isidharau nguvu ya sauti yake katika kulinda misingi ya demokrasia, uhuru na utawala wa sheria duniani, kuendelea kuishi kwa Chadema na ari na nguvu yake ya kuendelea na mapambano ni kipimo na ushahidi wa nguvu ya sauti ya IDU,” amesema Mbowe.

Katika hatua nyingine, Mbowe alisema katika kipindi cha Miaka Saba iliyopita Tanzania ilikuwa kwenye Siasa za giza na Utawala wa mabavu ambapo umesababisha madhara makubwa kwa Chadema ikiwemo vifo, majeruhi, walemavu na hata wakimbizi ambavyo vyote vimesababishwa na msukumo wa kisiasa.

“Kama ambavyo imesharipotiwa mara kadhaa, Demokrasia, Utawala wa Sheria na Haki za Binadamu zimekuwa kifungoni kwa miaka saba nchini Tanzania, tumekuwa katika utawala wa kimabavu na Chama cha Chadema kimekuwa mhanga mkubwa wa utawala huo,” alisema Mbowe.

“Ari yetu ipo na imeendelea kuwa imara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba pamoja na kusimama imara kupigania misingi tunayoiamini, lakini marafiki zetu wa kimataifa mkiwemo wa IDU mmekuwa nasi na bado mnaendelea kusimama na sisi.”

Katika hatua nyingine, Mbowe alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu mbalimbali wa nchi na Taasisi za Kimataifa kutafuta uungwaji mkono wa jitihada za Chadema katika kurudisha Demokrasia Tanzania kupitia Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Mbowe anatarajiwa kurejea nchini Disemba 12, 2022

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!