Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Morocco yatinga nusu fainali, Ronaldo amwaga chozi
MichezoTangulizi

Morocco yatinga nusu fainali, Ronaldo amwaga chozi

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Morocco imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia baada ya kuiondoa timu ya Taifa ya Ureno kwa bao 1-0 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Barani Afrika kutinga nusu fainali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Morocco ambayo ndio timu pekee kutoka Barani Afrika iliyokuwa imetinga katika hatua hiyo ya robo fainali, leo tarehe 10 Disemba, 2022 imeipeperusha vyema bendera ya Bara hilo baada ya kuichapa Ureno bao 1-0 huko nchini Qatar.

Bao la Morocco lilitumbukizwa kimyani na straika matata Youssef En-Nesyri anayekipiga katika klabu ya Sevila ya Hispania, dakika ya 42 ya mchezo huo.

Licha ya Ureno kupeleka mashambulizi mara kwa mara langoni mwa Morocco, wawakilishi hao waliweka ukuta wa kipekee hadi dakika 90 zilipokamilika.

Hata hivyo, dakika ya 93 ya mchezo huo Morocco ilipata mzigo mzito wa kuzuia baada ya mshambuliaji wake Walid Cheddira anayekipiga katika klabu ya Bari inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia kulimwa kadi nyekundu.

Baada ya mchezo huo staa wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye aliingia kipindi cha pili kuliokoa taifa lake, aliondoka uwanjani na kuelekea moja kwa moja vyumbani huku akimwaga machozi hasa ikizingatiwa historia yake katika michuano hii yamkini imefikia tamati kutokana na umri wa miaka 37 alionao sasa.

Kwa matokeo hayo Morocco wanasubiri mshindi kati ya Ufaransa na England ambao watapepeta leo saa nne usiku.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Bunge lalia msongamano wa mizigo bandari Dar es Salaam

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!