Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya DC Mpogolo ahamasisha chanjo ya polio
Afya

DC Mpogolo ahamasisha chanjo ya polio

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, Edward Mpogolo amewataka wazazi wenye watoto wenye umri chini ya miaka mitano wawapeleke kupata chanjo ya polio awamu ya nne, inayotolewa wilayani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Mpogolo amesema hayo jana tarehe 2 Disemba, 2022 baada ya kushiriki zoezi la utoaji chanjo hiyo katika Hospital ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Amesema wazazi wanawajibu wa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hiyo, ili kuwakinga dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio).

DC Mpogolo aliendelea kusisitiza kuwa Serikali imejipanga kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo polio na kwamba watoa huduma ya afya na chanjo ya polio wanapita kutoa elimu kwa kila kaya juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio) lengo ni kuwalinda watoto wote wawe salama maana ni taifa la kesho.

Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya, Dk. Alex Alexander amesema timu ya wataalamu huduma ya chanjo ya polio imesambaa karibu vijiji vyote kutoa elmu juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kupooza (polio) huku wakiakikisha mtoto chini ya umri wa miaka mitano anapata chanjo hiyo.

Mratibu wa Chanjo Wilaya ya Same, Happinus Pilula amesema hospital ya wilaya imejipanga kikamilifu kuhakikisha zoezi hilo la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano linakamilika na kuakikisha kila mtoto anapata chanjo hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!