Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wana Musoma waipongeza Serikali kwa kuwapiga ‘jeki’ wavuvi
Habari za Siasa

Wana Musoma waipongeza Serikali kwa kuwapiga ‘jeki’ wavuvi

Spread the love

WAVUVI katika Ziwa Victoria upande wa  Halmashauri ya Wilayani Musoma, mkoani Mara, wamepongeza hatua ya Serikali kutoa mikopo isiyokuwa na riba kwa ajili ya kuboresha shughuli zao, wakisema itasaidia kuwainua kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Pongezi hizo zilitolewa jana katika zoezi la usajili wavuvi katika Jimbo la Musoma Vijijini,wanaotaka kupata mikopo hiyo inayotolewa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, imetoa taarifa ya kupongeza utolewaji mikopo hiyo, ikisema itasaidia kuanzisha uvuvi wa kisasa wa vizimba, wenye uvunaji mkubwa wa samaki.

“Samaki wamepungua sana kwa hiyo uamuzi wa Serikali kutoa mikopo isiyokuwa na riba ni uamuzi mzuri sana kwani mikopo hiyo itaenda kubadili mtindo wa uvuvi ndani ya ziwa hilo.Wavuvi wa Musoma wenye uzoefu mkubwa wamejitokeza kwa wingi kuomba mikopo hiyo kutoka serikalini,” imesema taarifa ya Ofisi ya Profesa Muhongo.

Mathias Peter amempongeza Rais Samia kwa kufanya  kitendo hicho kwa mara ya kwanza na kuifanya sekta ya uvuvi kuaminiwa na taasisi za kifedha.

“Serikali ya Rais Samia imeonesha dhamira njema ya kutujali wavuvi, tunaipongeza sana. Ni mara ya kwanza sekta ya uvuvi kuwekewa fedha na wavuvi kuaminiwa kuweza kukopeshwa. Mikopo hii itasaidia wavuvui kuachana na dhana za kizamani za uvuvi na kutumia dhana za kisasa. Pia tunampongeza mbunge wetu kwa kutusaidia ili tuweze kupiga hatua katika kazi zetu,” alisema Mathias.

Naye Mkazi wa Kata ya Kiriba, wilayani humo, Jane Joseph amesema mikopo hiyo italeta mageuzi katika shughuli za uvuvi wa samaki hususan kwa wanawake.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ukuzaji katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, amesema halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri zinazonufaika na mikopo hiyo, ambayo Serikali ya Rais Samia amezipata kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), kuboresha sekta ya uvuvi.

Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na umri wa miaka 400,000, ujazo wa maji kilomita za ujazo 2,424 na aina 500 za samaki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!