Saturday , 18 May 2024
Home Kitengo Michezo NMB yadhamini milioni 25 michuano ya Golf- Lugalo
Michezo

NMB yadhamini milioni 25 michuano ya Golf- Lugalo

Spread the love

BENKI ya NMB imetoa udhamini wa Sh. milioni 25 kwa Mashindano ya Gofu ya Mkuu wa Majeshi Tanzania (NMB CDF Trophy 2022), kama muendelezo wa sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambayo hufanyika Septemba mosi.

Sherehe za kumbukumbu hizo kwa mwaka huu yamelazimika kusogezwa kwa mwezi mmoja kutokana na sababu mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza wakati akipokea mfano wa hundi Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo, ameishukuru  Benki ya NMB kwa kuwa mdhamini wa muda mrefu na kufanyia maboresho zaidi kwa mwaka huu.

Alisema timu mbalimbali zimethibitisha kushiriki michuano hiyo, ambayo itahusisha makundi ya Watoto (junior), Madaraja (division) ya A, B, na C, pamoja na wanawake na Seniors.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Wateja Maalum wa Benki ya NMB, Getrude Mallya, alisema benki yake imedhamini mashindano hayo kwa Sh. milioni 25.

Pia aliwaalika viongozi wa  klabu ya gofu Lugalo kushiriki mbio za NMB Marathon 2022  ‘Mwendo wa Upendo’ zitakazofanyika Oktoba 1, 2022 katika viwanja vya Leaders Club kwa lengo la kukusanya Sh. milioni 600 za kusaidia matibabu ya kina mama wenye matatizo ya fistula nchini.

Mashindano ya Gofu yatafanyika Oktoba 1 hadi 2 mwaka huu kwenye Viwanja vya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Uingereza, Hispania, Italia na Ufaransa kinawaka leo

Spread the loveLIGI mbalimbali barani ulaya kuendelea leo na michezokadhaa mikali itakwenda...

Michezo

Leo mkwanja upo Meridianbet, usipishane nao

Spread the love  Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Michezo

Anza wikendi yako na Meridianbet, upige mkwanja wa maana

Spread the love Siku ya leo ni nzuri sana kwa wewe mtumiaji...

Habari MchanganyikoMichezo

Arafat atoka bima na kurejea kwenye benki

Spread the loveRais wa Zanzibar Hussein Mwinyi amemteua Arafat Ally Haji kuwa...

error: Content is protected !!