Sunday , 28 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Waandamana kupinga mawakili wanaowatetea watuhumiwa wa kufuru Pakistani
Kimataifa

Waandamana kupinga mawakili wanaowatetea watuhumiwa wa kufuru Pakistani

Spread the love

MAKUNDI ya wafuasi wa Dini ya Kiislam na wafanyabiashara nchini Pakistani wameandamana kupinga watuhumiwa wa makosa ya kumdhihaki Mtume Muhammad (S.A.W) ‘kufuru’ jijini Khyber Pakhtunkhwa wasipate utetezi Mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Maandamano hayo yalifanyika wiki iliyopita katika soko kuu la wilaya ya Battagram na Ahle Sunnat Wal Jamaat, Jamaat-i-Islami, Jamiat Ulema-i-Islam-Fazl na wafanyabiashara.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari cha Dawn, miongoni mwa watuhumiwa wa makosa hayo ni Ofisa wa zamani wa Frontier Constabulary aliyekamatwa na kuzuiliwa chini ya kifungu cha 295-C cha Kanuni ya Adhabu ya Pakistani, chini ya kufuru.

Maandamano hayo yaliongozwa na rais wa mkoa wa ASWJ, Maulana Atta Mohammad Deshani, Katibu Mkuu wa JUI-F Maulana Faridudin, Jamaat-i-Islami Hafiz Rasheed Ahmad, viongozi wa wafanyabiashara Shah Hussain, Abdul Ghaffar Deshani na Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Wanasheria wa Wilaya ya Battagram, Ziaullah Khan.

Walisema familia za watuhumiwa hazikuguswa na kwamba wameishinikiza Mahakama itoe idhabu ya mfano kwao.

Walisema iwapo polisi watatoa nafuu kwa washukiwa au kufanya uchunguzi mbovu, mawakili hao watawafikisha mahakamani.

Wanaharakati wanadai kuwa sheria hiyo inatumika vibaya ambapo inawaadhibu wachache.

Wanaeleza kuwa makundi ya walio wachache nchini Pakistani wanauawa kila mara na kufanyiwa ukatili wa kinyama kwa jina la kufuru, kuingia Uislamu na tofauti nyingine za kimadhehebu.

Kwa mujibu wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Pakistani, kesi za kukufuru si mpya nchini Pakistani. Takriban watu 585 waliwekwa kizuizini kwa tuhuma za kukufuru mwaka 2021, na idadi kubwa ya watu kutoka Punjab,

Pakistani ilitunga sheria za kukufuru baada ya kugawanyika na India mwaka 1947.

Hata hivyo, wakati wa utawala wa Jenerali Zia-ul Haq kati ya 1980 hadi 1986, vifungu kadhaa vilianzishwa ambavyo vilijumuisha kifungu cha kuadhibu kufuru dhidi ya Mtume Muhammad (S.A.W) na adhabu ya jambo hilo ilikuwa kifo au kifungo kwa maisha.

Kulingana na takwimu za Tume ya Kitaifa ya Haki na Amani, Waislamu 776, Waahmadiyya 505, Wakristo 229 na Wahindu 30 wamefungwa chini ya sheria ya kukufuru kuanzia 1987 hadi 2018. (ANI).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

error: Content is protected !!