Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko DC Dodoma: Waliokatiza masomo rudini darasani
Habari Mchanganyiko

DC Dodoma: Waliokatiza masomo rudini darasani

Spread the love

 

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Shekimweri Jabiri amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanapeleka watoto wao shule hususani walioshindwa kuendelea na masomo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mkuu wa wilaya hiyo ametoa kauli hiyo leo tarehe 8 Septemba, 2022 kwenye kilele cha maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima iliyofanyika katika uwanja wa sanamu ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dodoma.

Shekimweri amesema kuwa wapo baadhi ya watoto wengi ambao wameshindwa kuendelea na masomo na wengine kukataliwa na mfumo wa kujiunga na elimu ya msingi au sekondari lakini kwa sasa kwa kutumia mfumo wa elimu ya watu wazima wanahaki ya kuendelea na masomo.

“Ukitaka kuendelea kutawala watu, kuwaonea watu na kushindwa kuwapatia huduma muhimu na wasilalamike… wanyime elimu.

“Lakini kwa kuliona hilo Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kuwa watoto wote ambao waliokatisha masomo yao iwe kwa bahati mbaya au kwa changamoto yoyote ya kimaisha basi anayo fursa ya kuendelea na masomo sasa” ameeleza Shekimweri.

Aidha, amesema kitendo cha kumnyima mtu yoyote elimu ni kitendo cha kumtengenezea umasikini kwani hata maandiko matakatifu yanahimiza kuishika sana elimu.

Pamoja na hayo Mkuu huyo wa wilaya amesema kwa wilaya ya Dodoma sasa imefanikiwa kuwapatia elimu wanafunzi 50 waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali jambo ambalo amesema ni maendeleo lakini bado jitihada kubwa za kuwapata wengine zinaendelea.

“Wapo watoto wengi walioshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali, wengine walibakwa, wengine uchumi na wengine ni changamoto ya ujana balehe.

” Kwa maana hiyo watu wa elimu wanatakiwa kuendelea kutafuta uwezekano wa kuwapata watoto ambao wanahitaji kuendelea na masomo kwa lengo la kujiendeleza,” ameeleza Shekimweri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!