Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Askofu Mchamungu: Mrema alikuwa kiongozi wa kipekee
Habari za SiasaTangulizi

Askofu Mchamungu: Mrema alikuwa kiongozi wa kipekee

Spread the love

ASKOFU Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Henry Mchamungu amesema kuwa Hayati Agustino Mrema alikuwa kiongozi wa kipekee kutokana uweledi aliouonesha katika nyadhifa mbalimbali alizozishika enzi za uhai wake ndani na nje ya Serikali. Anaripoti Juliana Assenga TUDARCo …  (endelea)

Mchamungu ametanabaisha hayo leo tarehe 24 Agosti, 2022  kwenye ibada ya mazishi ya mwanasiasa huyo mkongwe iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Agustine iliyopo Salasala jijini Dar es Salaam.

Katika mahubiri yake Askofu huyo amesema kuwa upekee wa mwanasiasa huyo, ulianzia alipokuwa Mbunge wa Moshi katika jimbo la Vunjo, kwa kuhakikisha watu katika eneo lake wanaishi katika mazingira mazuri kwa kutengeneza miundombinu imara.

“Mrema mwaka 1985 akiwa kama mbunge alijitahidi kuhakikisha watu walioishi katika eneo lake wanapata miundombinu bora hali iliyoimarisha maendeleo eneo hilo,” alisema Askofu huyo.

Ibada hiyo ya misa takatifu ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Fedrick Sumaye na wanasiasa mbalimbali.

Aidha, Askofu huyo aliendelea kusema kuwa enzi za uhai wake akiwa kama Waziri alipata sifa kubwa kwa kuanzisha vikundi mbalimbali vya ulinzi ili wananchi waishi kwa amani.

“Mrema kama waziri alikuwa shujaa katka usalama wa mambo ya ndani. Na ndipo kipindi cha utawala wake vikundi vya ulinzi shirikishi (sungusungu) vilipoanzishwa ili kuhakikisha watu wanaishi kwa amani na usalama,” alisema Askofu Mchamungu.

Mrema alifariki dunia tarehe 21 Agosti, 2022 katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alikuwa amelazwa tangu tarehe 16 Agosti, 2022 akipatiwa matibabu kutokana na matatizo ya mapafu.

Mwili wa mwanasiasa huyo mkongwe nchini unasafirishwa leo jioni kwenda Marangu mkoani Kilimanjaro ambapo utapumzishwa katika kijiji cha Kiraracha kesho tarehe 25 Agosti 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!