Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa RC Makalla aagiza mabasi yote kupita stendi ya Magufuli
Habari za Siasa

RC Makalla aagiza mabasi yote kupita stendi ya Magufuli

Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makala
Spread the love

 

MKUU wa mkoa Dar es salaam Amosi Makala awapa siku 14, kamanda wa kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamanda wa usalama barabarani wilaya ya Ubungo na wamiliki wote wa mabasi ya mikoani, kujadili suala la kushusha na kutoshusha abiria katika kituo cha Magufuli kisha kumpatia majibu. Anaripoti Juliana Assenga (UDSM) … (endelea)

Makalla ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa tarehe 12 Agosti, 2022, jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Ubungo kuhusu masuala mbalimbali ya mkoa huo.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka kujadili kuhusu suala hilo kwa uwazi bila kuongelea mambo yasio ya kweli na kusema yale yaliyosahihi na uhakika nayo kwa kurejelea taarifa zote walizonazo.

Kiongozi huyo amesema maamuzi na mapendekezo ambayo yatatolewa katika kikao hicho ndio ambayo yatamwezesha yeye kuyawasilisha kwa waziri ambaye ndiye mwenye dhamana na kumuomba kumsaidia.

Kwa sasa Amosi amesema anawahitaji wamiliki wote wa mabasi kuweza kushusha na kupitia katika kituo cha Magufuli mpaka pale ambapo maamuzi ya mwisho yatatolewa na Waziri Mkuu.

1 Comment

  • Asante ndugu makalla kwa kauli yako .lakini tunakuomba lolote utakalolipitisha au litakalo pitishwa lisiwe la muda liwe la kudumu na uwe na uwezo wa kufatiria kauli tupu haina mana yoyote kama hakuna mfatiriaji maana ya kusema ivyo nimeyaona kwa wafanya bishara ambao bishara zao wanapanga bara barani uliwazuia kwa muda sasa wanapaanga wamerudi tenaa na wanapanga bishara zao kihorerahole atujui kibari hiko cha kupanga bishara barabarani wamekipata wapi. Sasa walemavu wa macho hawajui wapite wapi vilema ambao wanatamba hawajui wapite wapi wenye maduka wanapo kuja wateja wao hawajui wapite wapi wenye magari hawajui wa paki wapi. Mkoa wa dsm umekuwa uko kihorerahole

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!