Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mpango atoa maagizo 6 Wizara, STAMICO, NEMC
Habari Mchanganyiko

Dk. Mpango atoa maagizo 6 Wizara, STAMICO, NEMC

Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango
Spread the love

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Philip Mpango ameagiza wizara ya Madini, STAMICO na NEMC kuongeza kasi ya ukaguzi maeneo ya uchimbaji madini katika kuzingatia uhifadhi wa mazingira. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Dk.Mpango ametoa maagiza hayo leo tarehe 12 Agosti 2022 jijini Dodoma katika maadhimisho ya miaka 50 ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) iliyokwenda sambamba na kauli mbiu isemayo “Tunajivunia kutimiza miaka 50 kwa kishindo.”

Dk.Mpango ametoa kauli hiyo kufuatia baadhi ya maeneo mengi ya uchimbaji wa madini kutozingatia uhifadhi wa mazingira hali ambayo husababisha watu wanaozungukwa na migodi kuvuta vumbi na kusababisha magonjwa na kugharimu maisha ya watu.

Hivyo ameagiza Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kuweka kipaumbele cha utunzaji wa mazingira na kutoa elimu kwa wachimbaji madini namna ya kujikinga na vumbi mahala za kazi.

Aidha,ametoa rai kwa taasisi za fedha kutoa mikopo yenye masharti nafuu ili wachimbaji wadogo waweze kupata fursa ya kupata mikopo na kuweza kupata vifaa vya kisasa vya uchimbaji madini huku akiitaka STAMICO kushirikiana na SIDO namna ya kutengeneza vifaa vyenye gharama nafuu.

Kuhusu ajira za watoto migoni Dk.Mpango ameagiza taasisi zinazohusika ziendee kukomesha suala hilo ili kulinda afya za watoto.

Naye Waziri wa Madini Dk.Doto Biteko amesema STAMICO limekuwa na mchango mkubwa katika kufufua maeneo ya uchimbaji madini yaliyofifia kutokana na kuacha kuendelezwa huku Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Seleman Jafo akisema wizara yake imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha sekta ya uchimbaji madini inakuwa rafiki katika utunzaji wa mazingira.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!