October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

RC Makalla aagiza mabasi yote kupita stendi ya Magufuli

Amos Makala, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

Spread the love

 

MKUU wa mkoa Dar es salaam Amosi Makala awapa siku 14, kamanda wa kikosi cha usalama barabarani kanda maalumu ya Dar es Salaam, kamanda wa usalama barabarani wilaya ya Ubungo na wamiliki wote wa mabasi ya mikoani, kujadili suala la kushusha na kutoshusha abiria katika kituo cha Magufuli kisha kumpatia majibu. Anaripoti Juliana Assenga (UDSM) … (endelea)

Makalla ametoa maelekezo hayo leo Ijumaa tarehe 12 Agosti, 2022, jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Ubungo kuhusu masuala mbalimbali ya mkoa huo.

Mkuu huyo wa mkoa amewataka kujadili kuhusu suala hilo kwa uwazi bila kuongelea mambo yasio ya kweli na kusema yale yaliyosahihi na uhakika nayo kwa kurejelea taarifa zote walizonazo.

Kiongozi huyo amesema maamuzi na mapendekezo ambayo yatatolewa katika kikao hicho ndio ambayo yatamwezesha yeye kuyawasilisha kwa waziri ambaye ndiye mwenye dhamana na kumuomba kumsaidia.

Kwa sasa Amosi amesema anawahitaji wamiliki wote wa mabasi kuweza kushusha na kupitia katika kituo cha Magufuli mpaka pale ambapo maamuzi ya mwisho yatatolewa na Waziri Mkuu.

error: Content is protected !!