Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari Ruto, Raila wachuana vikali matokeo ya awali
HabariTangulizi

Ruto, Raila wachuana vikali matokeo ya awali

Spread the love

 

Matokeo ya mapema yanaonesha kwamba mgombea wa Muungano wa Azimio Raila Odinga amekuwa akitatizika kupata asilimia 20 ya kura zilizopigwa katika maeneo mengi ya mlima Kenya ikiwemo Murang’a, Kiambu, Meru, Kirinyaga na kaunti nyingine zilizo na idadi kubwa ya kura katika eneo la Mlima Kenya. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa mashirika ya kimataifa… (endelea)

Katika kura iliyorekodi idadi ndogo ya wapiga kura, suala muhimu la ni nani ambaye atapata uungwaji mkono katika ngome ya mwingine ndio litaamua ni nani ataibuka mshindi.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Wafula Chebukati, hakutoa matokeo kuhusu kura ya Urais katika kituo kikuu matokeo ya Uchaguzi cha Bomas.

Hatahivyo Matokeo ya mapema ya kura za urais zilizotoka kutoka maeneo tofauti nchini yalionesha William Ruto akichuana kwa karibu na mpinzani wake mkuu Raila Odinga.

Huku wagombea wengine wawili George Wajackoyah na David Waihiga wakijipatia asilimia 0.5 ya jumla ya kura hizo kati yao, wagombea wawili wakuu wamekuwa wakibadilishana uongozi kufikia asilimia 50 ya kura zilizohesabiwa.

Kama ilivyotarajiwa Ruto alitawala katika majimbo ya Bonde la Ufa na Mlima Kenya, huku naye Odinga akipata uungwaji mkono kutoka Nyanza pamoja na eneo la Mashariki na Pwani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

Habari za SiasaTangulizi

Wizara Katiba na Sheria yaliomba Bunge Sh. 441.2 bilioni

Spread the love  WIZARA ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge liidhinishe bajeti...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!