October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto: Kenya ipo mbele sana uwazi katika uchaguzi

Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo cha nchini Tanzania, Zitto Kabwe, amesema Taifa la Kenya lipo mbele katika uwazi kwenye uchaguzi mkuu. Anaripoti Erick Mbarawa, TUDARCO…(endelea).

Zitto ambaye yupo nchini Kenya kwa shughuli za uangalizi wa uchaguzi leo Jumatano katika ukurasa wake wa twitter ameeleza kile alichokishuhudia na kufurahishwa na usimanizi, utendaji na uwazi kufuatia matokeo ya uchaguzi ambayo yanaendelea kutolewa.

Zitto amesema ameshuhudia matokeo ya kura zilizohesabiwa katika kituo cha Soy Primary School katika Jimbo la Soy yakitumwa kupelekwa katika kituo kikuu cha Taifa cha kuhesabu kura.

“Katika kituo cha Soy Primary School nilishuhudia matokeo yakitumwa moja kwa moja kutoka kituoni kwenda kituo kikuu cha Taifa cha kuhesabu kura. Kenya ipo mbele sana katika uwazi kwenye uchaguzi na hivyo kuipa heshima kura ya kila aliyepiga. Amesema Zitto.

Amesema alishuhudia hayo ikiwa ni zaidi ya asilimia 90 ya vituo vya kupigia kura vimewasilisha matokeo ya kura ya Rais katika kituo kikuu cha kuhesabia kura na fomu zikiwa mtandaoni ambapo kila mtu angeweza kuhesabu na kujua mshindi.

Mpaka sasa wapinzani wawili ambao ni Raila Odinga na William Ruto, ndio wapo kwenye mchuano mkali wa kuwania kiti cha Urais na hii ni kutokana na ushindani mkubwa walionao kwenye idadi ya kura ambazo zimehesabiwa mpaka hivi sasa.

error: Content is protected !!