BODI ya nafaka na mazao mchanganyiko nchini imewataka wakulima na wafugaji kuendelea kuzalisha kwa bidii kwani soko la mazao bado ni kubwa katika ukanda nchi za Afrika Masharikia na kati. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).
Rai hiyo imetokelewa na Ofisa kutoka bodi ya nafaka na mazao mchanganyika, Mhandisi Fredy Mbilinyi katika viwanja vya maonyesho ya wakulima nanenane jiji Mbeya.
Alisema mpaka sasa bodi hiyo imeshafungua vituo vya mauzo ya bidhaa kutoka Tanzania katika za Mji wa Juba nchini Sudani Kusini, Jamhuri ya Demokrasia watu wa Congo, Kenya na Zambia
Naye Waziri wa Mifugo, Mashimba Ndaki akiwa katika zoezi la kukagua na kuangalia mabanda ya maonyesho aliwataka watumishi umma kuwasaidia wakulima na kutoa elimu ili teknolokjia zinaonyeshwa zitolewa kwa wakulima ambao ndiyo walengwa wakuu.
Leave a comment