August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbarawa: Mikoa yote itaunganishwa kwa lami

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa

Spread the love

 

SERIKALI imepanga kufanya maendeleo katika maeneo mawili muhimu ya ujenzi na uchukuzi ikiwemo kuhakikisha inaunganisha makao makuu ya mikoa yote kwa barabara za lami. Anaripoti Juliana Assenga (UDSM) … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 4 Agosti, 2022, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa amesema ipo miradi mbalimbal inayotekelezwa ambayo ni ujenzi wa barabara na madaraja.

Kwa upande wa ujenzi wa barabara amesema zipo barabara ambazo zipo katika utekelezaji ambazo ni ujenzi wa kiwango cha lami barabara Njombe- Ndulambo-Makete yenye urefu wa kilometa 107.4.

Kwa upande wa madaraja amesema madaraja mbalimbali yaliyopo katika utekelezaji ambayo ni kama daraja la Wami maeneo ya Pwani, daraja la Gerezani lililopo Dar es salaam, na daraja la Kigongo-Busisi lililopo Mwanza.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa

Ametaja madaraja mengine saba ambayo yapo katika hatua za usanifu wa ujenzi ambayo ni Sukuma, Simiyu (Mwanza), Mtera (Dodoma), Mkenda (Ruvuma), Godegode (Kigoma), na Ugala(Tabora).

Kwa upande wa uchukuzi Mbarawa amesema Serikali imelenga katika kujenga na kukarabati meli, uboreshaji wa usafiri wa anga, uboreshaji wa bandari na uboreshaji wa mamlaka ya hali ya hewa.

“Mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imetenga kiasi cha Sh 2.135 trilioni ambapo kiasi cha Sh. 94.546 bilioni imetengwa kuweza kutumika katika matumizi ya kawaida na kiasi cha Sh 1.113 trillioni kuweza kutumika katika ujenzi wa reli ya kisasa,” amesema Mbarawa.

error: Content is protected !!