Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Michezo Simba SC kurejea nchini leo kuelekea ‘Simba Day’
Michezo

Simba SC kurejea nchini leo kuelekea ‘Simba Day’

Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba yenye makazi yake mitaa ya Msimbazi jijini Dar es Salaam wanatarajia kurejea nchini leo tarehe 4 Agosti, 2022, wakitokea nchini Misri walipokuwa wameweka kambi ya kujiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya NBC 2022/23 na mashindano ya kimataifa. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARco … (endelea).

Klabu hiyo iliondoka nchini tarehe 14 Julai, 2022, ikiwa na msafara wa wachezaji 19, wengine wakikwama kwasababu ya maswala ya viza na wengine wakiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa.

Aidha timu hiyo iliweka kambi Misri katika jiji la Ismailia na kucheza michezo minne ya kirafiki kwa ajili ya kupima kikosi chao kuangalia ubora na mapungufu.

Katika michezo hiyo minne waliyocheza waliweza kushinda michezo miwili,sare moja, na kupoteza mchezo mmoja na timu walizo fanikiwa kucheza nazo ni pamoja na Isimaila FC , AL-Kholood Club , Haras El Hodoud.

Aidha timu hiyo itarejea leo inchini kwa ajili ya maandalizi ya Simba Day itakayofanyika tarehe 8 Agosti, 2022 katika dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Siku hiyo ni maalumu kwa ajili ya kutangaza kikosi chao chote na benchi la ufundi ambapo kuna mabadiliko na maingizo mapya pia watakuwa na maandalizi kwaajili ya mechi ya ngao ya hisani dhidi ya mtani wake Yanga itakayopigwa tarehe 13 Agosti, 2022 katika uwanja wa Mkapa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Europa na Conference kukupatia pesa ndefu leo

Spread the love  ALHAMISI ya leo tutaenda kushuhudia mitanange ya kukata na...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Michezo

Usiku wa Ulaya umerejea kibabe kabisa

Spread the love  LIGI ya Mabingwa barani Ulaya imerejea tena na awamu...

Habari MchanganyikoMichezo

Mambo ya Ndani, Ulinzi zang’ara michezo ya Mei Mosi Arusha

Spread the loveRais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini...

error: Content is protected !!