August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea Kenya asafisha vyoo kushawishi wapiga kura

Spread the love

 

KUELEKEA Uchaguzi wa Kenya unaotarajiwa kufanyika Agosti 9, 2022 imezuka mishangao kwa wananchi mara baada ya baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuonekana wakitumia mbinu shawishi ili kuvutia wananchi hao kuwachagua. Anaripoti Erick Mbawala kwa msaada wa mashirika ya kimataifa … (endelea). 

Hii imedhihirika baada ya baadhi ya wagombea kuonekana wakijumuika katika shughuli za kawaida za kimaendeleo kwenye jamii ambazo hufanywa kila siku na wakazi wa maeneo husika kama vile kusafisha vyoo, kukata mbogamboga na kupika chai.

Moja kati ya wanasiasa ambaye ni mgombea wa kiti cha ugavana Nairobi, Polycarp Igathe, ameonekana amevaa ovaroli, buti na gravu kabla ya kuchukua ndoo yenye maji na kuanza kusafisha vyoo katika mji mkuu, Nairobi.

Pia Igathe amepigwa picha akiosha magari na kushiriki vinywaji katika vilabu vya burudani nyakati za usiku.

Watu wengi wameikejeli njia hiyo lakini Igathe ambaye ni mpinzani wa Seneta wa Nairobi, Johnson Sakaja, kwa upande wake ameona ni njia mojawapo ya uwajibikaji katika majukumu ya kulijenga taifa.

“Kwa muda mrefu imeonekana kama kazi chafu lakini hii ni kazi ya kuwajibika,” amesema Igathe.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wametaja hatua hiyo kama mbinu ya kuwashawishi wananchi kumchagua kuelekea uchaguzi huo na pia wametaja kuwa ni kama namna ya kujenga uhusiano mwema baina yake na wananchi.

error: Content is protected !!