Friday , 17 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Wapinzani Sri Lanka ‘washikana uchawi’
Kimataifa

Wapinzani Sri Lanka ‘washikana uchawi’

Spread the love

OMBWE la kisiasa nchini Sri-Lanka limeendelea kuivuruga nchi hiyo kwa siku ya pili mfululizo baada ya viongozi wa upinzani kushindwa kukubaliana nani atachukua nafasi zilizoachwa na viongozi waliokataliwa na wananchi. Inaripoti mitandao ya kimataifa… (endelea)

Hayo yanajiri wakati waandamanaji nchini humo wanaendelea kukaa katika makazi na ofisi ya Rais Gotabaya Rajapaksa na ya waziri mkuu tangu tarehe 9 Julai, 2022 wakishinikiza viongozi hao waondoke madarakani na wameapa kuendelea kubakia hadi pale viongozi hao watakapojiuzulu rasmi.

Waziri mkuu  wa nchi hiyo ya iliyopo kusini mwa Asia, Ranil Wickremesinghe alisema ataachia ngazi pale serikali mpya itakapochaguliwa na saa chache baadae spika wa bunge alitangaza kwamba Rais Rajapaksa atajiuzulu Jumatano.

Viongozi wa upinzani wamekuwa katika mazungumzo ya kuunda serikali mbadala itakayojumuisha vyama vyote na kiongozi mkuu wa upinzani Sajith Premadasa amependekezwa kuwa rais huku Dulla Allahperuma aliyekuwa waziri chini ya Rajapaksa, akipendekezwa kuwa waziri mkuu.

Viongozi hao wameaombwa kujadili watakavyogawana nafasi hizo kabla ya kukutana na spika wa bunge leo jioni.

Aidha, mamilioni ya fedha za rupee yaliyoachwa na rais Gotabaya Rajapaksa nyumbani kwake baada ya kukimbia yatakabidhiwa mahakama hii leo Jumatatu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!