Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bosi NMB atunukiwa tuzo ya uongozi bora wa biashara Afrika
Habari Mchanganyiko

Bosi NMB atunukiwa tuzo ya uongozi bora wa biashara Afrika

Spread the love

AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ametunukiwa tuzo ya heshima ya uongozi bora wa biashara barani Afrika kwa uongozi wake shupavu wa taasisi hiyo kubwa ya fedha kuliko zote nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ruth ametunukiwa tuzo hiyo maalum ya “African Business Leadership Commendation Award” ya mwaka 2022 na jarida la African Leadership kwa juhudi zake za kuifanya NMB kuwa mstari wa mbele katika ujenzi wa taifa na kuchangia kikamilifu kuboresha maisha ya Watanzania.

Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa NMB – Kwame Makundi akipokea tuzo maalum ya uongozi wa biashara barani Afrika mwaka 2022 kutoka kwa Waziri wa Biashara Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza – Lord Dollar Popat kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna. Bi Ruth alitunukiwa tuzo hiyo na Jarida la African Leadership katika hafla iliyofanyika jijini London kwenye ofisi za Bunge la Uingereza juzi na kuwakilishwa na Bwana Kwame Makundi. Tuzo hiyo imemtambua Bi Zaipuna kama kiongozi shupavu na mahiri kwa uongoza wake na ubunifu katika sekta ya benki.

Jarida hilo linaloshapishwa na Taasisi ya African Leadership Organisation yenye makao yake makuu London nchini Uingereza, lina ushawishi mkubwa kimataifa na linaheshimika kwa kuyatangaza mafanikio ya bara la Afrika duniani.

Kwa mujibu wa mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa taasisi hiyo, Dk. Ken Giama, sababu zilizofanya Ruth kuibuka kidedea ni pamoja na uongozi wake uliotukuka na kuifanya NMB kuwa kinara wa ubunifu kwenye sekta ya benki nchini.

Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa NMB – Kwame Makundi akimkabidhi tuzo ya uongozi wa biashara barani Afrika mwaka 2022 – Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Ruth Zaipuna. Ruth alitunukiwa tuzo hiyo na Jarida la African Leadership katika hafla iliyofanyika jijini London kwenye ofisi za Bunge la Uingereza juzi na kuwakilishwa na Bwana Kwame Makundi. Tuzo hiyo imemtambua Bi Zaipuna kama kiongozi shupavu na mahiri kwa uongoza wake na ubunifu katika sekta ya benki

Dk. Giama amesema zaidi ya kuwa kiongozi mahiri na mwenye msimamo thabiti wa kibiashara, pia uongozi wake umechangia sana kusaidia NMB kutengeneza fursa nyingi za ajira na kuzalisha mali nchini na barani Afrika kwa ujumla.

“Umechaguliwa kwa kauli moja kutunukiwa tuzo hii maalum ya uongozi bora wa biashara barani Afrika na uteuzi wako unatokana na umahiri wako wa kuongoza na ubunifu katika sekta ya benki,” amesema Dk. Giami kwenye barua aliyomwandikia Ruth kuhusu kutunukiwa kwake tuzo hiyo.

Aidha, amesema ushindi wa Ruth ulitokana na mchakato makini unaozingatia sifa stahiki uliofanywa na timu ya uteuzi ya bodi ya wahariri wa Taasisi hiyo

Kiongozi huyo wa NMB alitunukiwa heshima hiyo wakati wa kilele cha mkutano wa maendeleo ya Afrika na Tuzo za Uongozi wa Biashara za Afrika (ABLA) zilizofanyika hivi karibuni kwenye Ukumbi wa House of Lords katika Bunge la Uingereza.

Akizungumza kabla ya kupokea zawadi ya Ruth wakati wa shughuli hiyo, Mkuu wa Idara ya Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa NMB, Kwame Makundi, alisema heshima hiyo ya kimataifa ina maana kubwa sana kwa Benki ya NMB na Tanzania kwa ujumla.

Aliwaambia washiriki wa hafla hiyotuzo hiyo ni ushahidi wa juhudi za makusudi ambazo uongozi wa Benki ya NMB umekuwa ukizingatia ili kuboresha maisha ya Watanzania na kusaidia maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Ruth alisema katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makundi kuwa tuzo hiyo haitambui tu mafanikio na mchango wake kama kiongozi bali pia unatambua mchango wa Serikali ya awamu ya sita na Benki Kuu ya Tanzania kuiwezesha NMB kustawi na kuendelea kuwanufaisha wadau wake wote.

“Ninashukuru kuwa kiongozi wa taasisi yenye sifa endelevu za kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi yanayochangia kubadili na kuboresha maisha ya watu wengi. Hili kwangu ni jambo kubwa sana.”

Taarifa kwa umma ya benki hiyo ilisema ushindi wa Ruth na washindi wenzake 10 wa tuzo za ABLA za mwaka huu zilizofanyika Julai 10 pia ni matokeo ya umakini wao wa kibiashara na mafanikio makubwa katika maendeleo ya sekta binafsi barani Afrika.

Mkutano wa Afrika ni moja ya programu muhimu za jarida la African Leadership unaowaleta pamoja viongozi wa taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Afrika, Ulaya na Marekani kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali kwa ajili ya mustakabli mpya wa bara hili na ulimwengu wote.

Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari inaonyesha mbali na Ruth wengine walioshinda tuzo za ABLA zilizotolewa Julai 4, 2022 ni Mfanyabiashara na Bilionea wa Lesotho Sam Matekane aliyeshinda tuzo ya heshima ya Maisha, Waziri wa Fedha wa Mauritius, Dk. Renganaden Padayachy.

Tuzo ya Kiongozi  bora wa Biashara Afrika ilienda kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Mitaji Nigeria, Dr Akintoye Akindele, Afisa Mtendaji Mkuu wa United Capital Plc ya Nigeria, Peter Ashade alishinda Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwaka 2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Nape aomba bajeti ‘kiduchu’ kwa mwaka 2024/25

Spread the loveWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Seneta: Wanasiasa hawasaidii mchakato wa Katiba mpya

Spread the loveSeneta wa jimbo la Busia, nchini Kenya, Okiya Okoiti Andrew...

Habari Mchanganyiko

Wananchi washauriwa kuongeza uelewa wa kujikinga na majanga

Spread the love WITO umetolewa kwa wananchi kuongeza uelewa na utayari kabla...

error: Content is protected !!