Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari Rasmi Mane amtikia Bayern
HabariMichezo

Rasmi Mane amtikia Bayern

Spread the love

 

MARA baada ya kuhudumu katika kipindi cha misimu sita, hatimaye klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza immemruhusu rasmi kuondoka kwenye klabu hiyo, mshambuliaji wake raia wa Senegal Sadio Mane. Anaripo Mwandishi Wetu…(endelea)

Mane amefikia maamuzi yakuondoka kwenye klabu hiyo ambayo amepata nayop mafanikio makubwa, mara baada ya kukataa kuongeza kandarasi mpya kutokana na mkataba wake kuelekea mwishoni.

Mshambuliaji huyo ametimkia kwenye klabu ya FC Bayern Munchen ya nchini Ujerumani, ambapo atakwenda kuchukua mikoba ya Robert Lewandowski ambaye mara baada ya msimu kukamilika alitangaza kuondoka klabuni hapo na kutafuta changamoto mpya.

Mchezaji huyo alijiunga na Liverpool akitokea kwenye klabu ya Southampton ya nchini Uingereza, ambapo katika msimu sita aliyocheza amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 120, katika mashindano yote, kwenye michezo 269 aliyocheza.

Akiwa ndani ya Liverpool Mane amefanikiwa kuipa taji la Ligi Kuu ya England klabu hiyo, mara baada ya kusubili kwa miaka 30, lakini pia alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya pamoja na kombe la FA.

Tayari klabu ya Bayern Munichen imeshamtambulisha rasmi mchezaji huyo, mara baada ya kumsainisha mkataba wa miaka mitatu ambao utamfanya akae ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2025.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za UEFA

Spread the love  HATIMAYE leo hii ndio kitaeleweka nani aende Nusu Fainali...

Michezo

Idris Sultan anogesha msimu wa 3 wa Bridgerton

Spread the loveSTAA wa burudani kutoka ardhi ya Tanzania, Idris Sultan amenogesha...

Michezo

Ligi mbalimbali za pesa kuendelea leo

Spread the love JUMAPILI ya leo imekaa kipesa tuu yani baada ya...

Michezo

Usiishie kuangalia tu game za leo, piga na mkwanja na Meridianbet

Spread the love  LIGI mbalimbali barani ulaya zitarejea tena Jumamosi ya leo...

error: Content is protected !!