Wednesday , 8 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge ashauri mabadiliko Sheria kuruhusu mifumo ya fedha ya Kiislamu
Habari za Siasa

Mbunge ashauri mabadiliko Sheria kuruhusu mifumo ya fedha ya Kiislamu

Mbunge wa jimbo la Wawi nchini Tanzania, Bakari Hamad Bakari
Spread the love

 

MBUNGE wa jimbo la Wawi nchini Tanzania, Bakari Hamad Bakari, ameitaka Serikali kufanya marekebisho ya Sheria ili kuruhusu mfumo wa fedha wa kiislamu kutumika nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mbunge huyo amesema mfumo huo unatumika na taasisi zaidi ya 400 kote duniani na kwamba nchi kama Nigeria na Uingereza zinatumia mfumo huo.

Akichangia hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka 2022/23 leo Jumatatu tarehe 20 Juni, 2022, Bakari amesema mfumo huo utasaidia kurahisisha ufadhili wa miradi kutoka katika nchi zinazotumia mfumo huo.

“Moja ya industry inayokuwa kwa kasi duniani ni Islamic Financing System na inakadiriwa taasisi zipatazo 400 duniani zinatumia mfumo huu lakini inakadiriwa ukuaji wa mfumo huo kwa mwaka ni asilimia 20,” amesema Bakari.

Amesema nchi nyingi hata zisizo za kiislamu zinatumia mfumo huo ikiwemo Afrika Kusini, Kenya, Nigeria na Uingereza na kwamba anaona haja ya Tanzania kuanza kutumia.

“Tunahitaji kufanya mabadiliko ya Sheria zetu ili kuruhusu mfumo huu mfano Sheria ya Benki ifanyiwe marekebisho ili kuutambua mfumo wa Islamic Financing,” amesema.

Ameongeza pia kuna haja ya kufanyia marekebisho Sheria ya Bima ili kuwezesha Takaful kama Islamic Insurance ya kutatua matatizo mbalimbali ya bima za kiislamu.

Pia amesema mabadiliko yafanyike kutambua mfuko wa dhamana wa kiislamu (Islamic Bond) akitiolea mfano Sukuk ili kuweza kufadhili miradi mbalimbali.

Alisema jambo hilo lipo kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwamba kufikia 2025 itakuwa imeanzisha mfumo huo wa fedha wa kiislamu.

Alisema ipo hofu imejengeka katika jamii kuhusu mfumo huo na kuwatoa hofu watanzania kuwa huo ni mfumo kama ilivyo mingine.

“Hapa Tanzania tunayo mifumo mingi ya kifedha ya kiislamu lakini inatumika kwa watu wote, sambamba na uwepo wa shule na hospitali ambazo zinatumika kwa watu wote bila kubaguana,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

Habari za SiasaTangulizi

Samia: Kuanzia Agosti marufuku kutumia mkaa, kuni

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mwendokasi Kigogo – Segerea kujengwa awamu ya 5

Spread the loveNaibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Festo Dugange...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Rais Samia ni Mzanzibari: Shida Iko Wapi?

Spread the loveTAIFA linakabiliwa na upungufu wa fikra sahihi. Upungufu huu unaonekana...

error: Content is protected !!