July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mpina alilia kamati ya Bunge kuchunguza Bwawa la Nyerere

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina

Spread the love

 

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpinga, ameliomba Bunge liunde tume kwa ajili ya kuchunguza masuala mbalimbali yenye tija kwa taifa, ikiwemo Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwalimu Julius Nyerere na malimbikizo ya kodi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mbunge huyo wa kisesa, ametoa ushauri huo leo Jumatatu, tarehe 20 Juni 2022, bungeni jijini Dodoma, akichangia makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.

Kuhusu mradi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Julius Nyerere, Mpina amedai “Kuna maeneo muhimu lazima tuunde tume ya Bunge na Spika, Dk. Tulia Ackson nakuomba ukubali utanishukuru utakayoenda kuona, jambo moja naomba liundiwe tume ni ucheleweshaji wa ukamilishaji mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere,” amesema Mpina.

Katika hatua nyingine, Mpina ameshauri Bunge liunde tume kwa ajili ya kuchunguza malimbikizo ya kodi, pamoja na kesi za kikodi zilizoko mahakamani, akidai taifa linapoteza matrilioni ya fedha kutokana na changamoto hiyo.

“Tuangalie suala la malimbikizo ya kodi, hivi ni kweli taasisi za kodi zinafikia malimbikizo ya trilioni 7.54? Kodi mnashindwa kukusanya halafu uwezo wa kukusanya ukawa asilimia 10 halafu tunakaa kimya katika hili?”

“Hili jambo lazima malimbikizo ya kodi na mapingamizi yaliyoko kwenye mahakama, ni muhimu yaundiwe tume, sababu Serikali kila tukiiambia haitekelezi hilo,” amesema Mpina.

Wakati huo huo, Mpina amelishauri Bunge liunde tume kwa ajili ya kuchunguza sababu za kupanga kwa bei za mafuta na mbolea nchini, akidai ongezeko hilo linasababishwa na hujuma mbalimbali.

“Iundwe tume kuchunguza kupanda bei ya mafuta, kwa kisingizio cha vita ya Ukraine na Russia na tuweze kujua yale makando kando mengine yaliyomo humo ndani ambayo mchezo uliofanya bei kupanda nchini,” amesema Mpina na kuongeza:

“Pia, iundwe tume kuchunguza bei za mbolea nchini na biashara inavyofanya tulikuwa tunafanya vizuri sana zamani, tulikuwa na viwanda vinavyozalisha mbolea, tuna ule mfumo wa kuagiza mbolea leo hii mfumo umeuawa. Tuchunguze hizi bei zinazopanda zina uhalisia.”

error: Content is protected !!