July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sijawahi kupata heshima kama hii: Prof. Kabudi amshukuru Samia

Mbunge wa jimbo la Kilosa nchini Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi

Spread the love

 

MBUNGE wa jimbo la Kilosa nchini Tanzania, Profesa Palamagamba Kabudi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa Timu Maalumu ya Rais ya Majadaliano ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mbunge huyo ambaye amewahi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pia alikuwa Mweyekiti wa Timu ya Tanzania katika majadiliano na kampuni ya Barrick Gold Corporation kuhusu mgogoro na Kampuni ya Acacia Mining.

Kabudi ametoa shukrani hizo leo Jumatatu tarehe 20 Juni, 2022 bungeni jijini Dodoma akichangia hoja ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23.

“Mheshimiwa Rais amenipa heshima kubwa sana ambayo sitaisahau katika maisha yangu yote ya kuwa duniani,” amesema na kuongeza; “sijawahi kupata heshima kama hiyo.”

Akichangia hotuba ya bajeti kuu ya Serikali amepongeza hatua ya Waziri wa Fedha kusamehe kodi ya kuhamisha mtaji (capital gain tax) nakusema itarahisisha utekelezaji wa mikataba mipya ya ubia wa Serikali na makampuniya madini.

Amesema zipo aina mbili za ubia wa kampuni ambazo ni hisa zinazoisha na ile yah isa zisizokwisha endapo mwekezaji hatoongeza mtaji.

Amesema Tanzania imechagua mikata ya hisa zisizokwisha ambapo ina asilimia 16 zitakazobakia hivyo katika kipindi chote cha utekelezaji wa mkataba huo.

Amesema zipo nchi nyingi zilizoingia mikataba yah isa zinazokwisha ambazo zilianza na asilimia 50 lakini zimeshuka hadi kuisha kabisa kwa kushindwa kuongeza mtaji.

Amesema jambo lingine lililofanyika ni kuunda kampuni za ubia na makampuni ya madini na kuanzisha kapuni za ubia ambazo ndizo zinazomiliki leseni ya uchimbaji.

Amefafanua huko nyuma Serikali ilikuwa ikimiliki rasilimali lakini makampuni yalikuwa yanamiliki leseni za madini.

error: Content is protected !!