KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imeshauri mambo saba kuhusu deni la taifa “pamoja na kwamba deni hilo ni himilivu.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)
Hadi mwezi Machi 2022, deni la Serikali lilikuwa ni Sh69.44 trilioni ukilinganisha na Deni la mwezi Machi 2021, la Sh64.46 trilioni Sawa na ongezeko la asilimia 7.73 (Sh4.98 trilioni).
Akiwasilisha taarifa ya Kamati ya Bajeti leo Alhamisi tarehe 16 Juni 2022, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Daniel Sillo amesema wanaishauri Serikali kuangalia uwezekano wa kujipima uhimilivu wa deni kwa kutumia kiashiria cha makusanyo ya mapato ya ndani kwa ulipaji wa deni.
“Hii ni kwa sababu deni la Serikali hulipwa na makusanyo ya ndani na ni malipo ya lazima (first charge) katika matumizi ya Serikali,” amesema.
Kwa kuwa Tanzania ilipata The Debt Service Suspension Initiatives– DSSI toka benki ya Exim ya China (US$ 99.5 million) na French Development Agency (US$2.6 million), kamati imeishauri Serikali kulipa madeni haya mara tu muda wa kulipa utakapofika ili kuondoa tatizo la malimbikizo ya madeni
Pia imeishauri kukamilisha haraka mchakato wa kufanyiwa tathmini ya uwezo wa ukopaji na ulipaji (credit rating) ili kuiwezesha Serikali kupata mikopo yenye masharti nafuu na kwa urahisi
Mbali na hayo Kamati uimeshauri mikopo yenye masharti ya kibiashara ielekezwe katika miradi yenye sura ya kibiashara, kuboresha mikakati ya kukusanya kodi, kutafuta mikopo yenye masharti ya kati na izingatiwe kwamba gharama za mikopo ya biashara zitaongezeka kutokana na kuongezeka kwa riba za mikopo katika mataifa yaliyo endelea pamoja na mfumuko wa bei.
Leave a comment