Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yatoa gawio bilioni 30, Dk. Mpango kumfikishia salamu Rais Samia
Habari Mchanganyiko

NMB yatoa gawio bilioni 30, Dk. Mpango kumfikishia salamu Rais Samia

Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania wamekabidhi Sh30.7 bilioni kwa Serikali huku Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango akisema benki hiyo imefanya siku yake na Serikali nzima kuwa yenye furaha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Dk. Mpango amesema hay oleo Jumatano tarehe 15 Juni 2022 wakati akipokea gawio hilo kutoka NMB jijini Dodoma ikiwa ni ongezeko la Sh.10 bilioni ikilinganishwa na gawio walilotoa mwaka jana la Sh.20.8 bilioni ambayo ilikuwa ni faida ya 2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Dk Philip Mpango (wapili toka kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 30.7 kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna (watatu toka kulia). NMB jana ilikabidhi hundi hiyo ikiwa ni Gawio kwa Serikali yaliyofanyika jana Jijini Dodoma ,wengine katika Picha kulia kabisa ni Waziri wa Fedha na Mipango ,Dk.Mwigulu Nchemba ,kutoka kushoto ni Afisa Mkuu wa fedha NMB Juma Kimori na wapili toka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB ,Dk Edwin Mhede .

Gawio hilo limetolewa ikiwa ni faida ya NMB kwa mwaka wa fedha ulioishia 2021 ambapo Sh.Sh97 bilioni zilipitishwa na mkutano mkuu wa wana hisa wa NMB kutolewa kwa wanahisa kama gawio.

Serikali inayomiliki hisa asilimia 31.8, imepokea Sh.30.7 bilioni kama gawio lake kutoka Benki ya NMB ikiwa ni ongezeko la asilimia 40 ukilinganisha na mwaka jana.

Kwa gawio hilo, Benki ya NMB ndani ya kipindi cha miaka mitano kuwa wametoa Sh80.544 bilioni kwa serikali.

Akipokea mfano wa hundi ya kiasi hicho, Dk. Mpango amesema benki hiyo imeendelea kuiheshimisha Serikali kwa kuonyesha namna gani inavyokuwa kimtaji na kuwajali wateja wake.

Hata hivyo, Dk Mpango ameagiza kwa benki hiyo kuongeza ubunifu ili iweze kuwafikia watu wengi vijijini, kuwa benki bora na kusaidia ajira kwa vijana ikiwemo utunzaji mazingira.

“Hata nitakapokwenda kumpokea Mheshimiwa Rais, hili litakuwa ni jambo la kwanza kumuambia, moyo wangu umeburudika sana, mmenifurahisha sana nasema hongereni sana,” alisema Dk Mpango.

Akitoa taarifa yake kwa Makamu wa Rais, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna amesema faida ya benki baada ya kodi katika kipindi cha 2021 iliongezeka kwa asilimia 41 hadi kufikia Sh290 bilioni.

Kiasi hicho ni kikubwa ukilinganisha na Sh206 bilioni ya mwaka 2020 ambapo idadi ya idadi ya akaunti za wateja iliongezeka hadi kufikia milioni tano ikilinganishwa na milioni nne za 2020.

“Katika kuhakikisha Benki inaendelea kuwa na maendeleo endelevu, tumeweza kuongeza mtaji wa Benki hadi Sh1.3 trilioni na Benki iliendelea kuwa na ufanisi, na kuweka rekodi ya uwiano wa gharama za uendeshaji na mapato, kufikia asilimia 46,” alisema Zaipuna.

Afisa huyo amesema kwa mwaka 2021, Benki ilipata Tuzo saba za kimataifa, ikiwemo ya benki bora nchini kwa mwaka wa tisa mfululizo ambayo iliyotolewa na Jarida la Kimataifa la Euromoney. Kwa mujibu wa Mtendaji huyo, hadi mwishoni mwa 2021, jumla ya mikopo ya Sh4.3 trilioni ilikuwa imetolewa kwa wakulima, wafanyabiashara wadogowadogo na wa Kati na watu binafsi.

Akizungumzia mafanikio ya benki, alisema yalitokana na uwekezaji katika mifumo ya kidijitali, huduma za wakala, ambazo ziliongezeka na kufikia mawakala 10,194 ukilinganisha na 8,410 waliokuwepo 2020.

Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya NMB, Dk Edwin Mhede alisema ongezeko la faida kwa benki hiyo linatokana na uimara na umadhubuti wa uongozi na kwamba wanajivunia kuwa na Mtendaji Mkuu Ruth Zaipuna.

Alitaja mafanikio kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kuwa yamekuwa yakipanda kila mwaka ambapo 2020 walitoa gawio la Sh20.8 bilioni, huku 2019 zikiwa Sh15.6 bilioni.

Dk Mhede amesema gawio kwa mwaka wa 2022 wanatarajia kuwa na gawio nono zaidi kwani kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wamepata faida kubwa inayolingana na faida ya mwaka mzima katika kipindi cha miaka ya nyuma kutokana na ubunifu uliofanywa na watumishi wa benki.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!