Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Masauni alitaka jeshi la uhamiaji kufuata sheria uingiaji, utokaji wageni
Habari Mchanganyiko

Masauni alitaka jeshi la uhamiaji kufuata sheria uingiaji, utokaji wageni

Spread the love

 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yusufu Masauni ameitaka Idara ya Uhamiaji nchini kusimamia uingiaji na utokaji wa wageni katika mipaka ya nchi kwa kufuata sheria za nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Waziri Masauni ameyasema hayo leo Jumatano tarehe 15, Juni, 2022 Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha alipofika kukagua maendeleo ya zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.

Aidha, Masauni amebainisha kuwa serikali itafanya uhakiki wa kina kubaini uendeshaji wa Asasi za Kiraia nchini kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na zile zitakazokiuka zitachukuliwa hatua kali za kisheria.

Masauni ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya zoezi la uwekaji alama na kuwataka wahusika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mwalimu Raymond Mangwala aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela, alimueleza Masauni kuwa amepokea maelekezo yake na kwamba atahakikisha kuwa hali ya usalama wa wananchi na mali zao inaendelea kuimarishwa wilayani Ngorongoro na kuwa zoezi hilo litaendelea kwa hali ya amani na utulivu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!