Wednesday , 8 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Mpango aagiza mashirika kutoa gawio kwa Serikali
Habari Mchanganyiko

Dk. Mpango aagiza mashirika kutoa gawio kwa Serikali

Spread the love

MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, ameagiza mashirka yote yanayotakiwa kutoa gawio kwa Serikali kufanya hivyo mara moja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia ameagiza Taasisi zinazotakiwa kutoa asilimia 15 ya mapato ghafi kwa mujibu wa sheria zifanye hivyo kikamilifu na kwa wakati.

Makamu wa Rais amesema hayo leo tarehe Jumatano tarehe 15, Juni 2022, wakati wa hafla ya kupokea Gawio la Sh 30.7 bilioni kutoka kwa Benki ya NMB iliofanyika katika Ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.

Dk. Mpango amesema Mashirika ambayo yanategemea ruzuku kutoka mfuko mkuu wa Serikali yanapaswa kuwa na mikakati madhubuti na inayotekelezeka ya kupunguza utegemezi kwa Serikali na kumuagiza msajili wa Hazina kuhakikisha wakuu wa taasisi husika wanatekeleza maagizo hayo.

Aidha Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuimarisha na kuweka mazingira rafiki na endelevu ya kufanya biashara katika sekta ya fedha na sekta zote nchini.

Pia ameipongeza Benki ya NMB kwa kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii nchini (corporate social responsibility) sambamba na kusaidia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato.

Amewataka kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuongeza fursa za ajira kwa vijana na wanawake pamoja na kuboresha huduma za kijamii kwenye sekta mbalimbali kama afya,elimu na utunzaji wa mazingira ikiwa ni pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na tabiawatu.

Kwa Upande wake Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba amesema Wizara itaendelea kusimamia maelekezo ya kuhakikisha taasisi za serikali na zile ambazo serikali ina hisa zinatoa Gawio.
Aidha amesema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi zote za sekta binafsi ili kuweza kuhakikisha zinafanya kazi vizuri.

Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema Gawio la Serikali kutoka Benki ya NMB limeendelea kukua kila mwaka na kuwa endelevu mpaka kufikia Sh 30.7 bilioni kwa mwaka 2022 kutoka Sh 10.48 bilioni mwaka 2018.

Amesema azma ya NMB ni kuleta tija kwa wawekezaji ikiwemo serikali ambayo inamiliki hisa za asilimia 31.8.

Aidha Bi Zaipuna ameongeza kwamba Benki ya NMB itaendelea kuwa mdau mkubwa wa serikali katika kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi hasa kupitia uwekezaji katika sekta ya kilimo na biashara.

Amesema hadi mwezi Desemba 2021 jumla ya mikopo ya Sh. 4.3 Trilioni imetolewa kwa wakulima na wafanyabiashara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

error: Content is protected !!