WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itapunguza tozo ya muamala kutoka kiwango kisichozidi Sh. 7,000 hadi kiwango kisichozidi Sh. 4,000 . Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 14 Juni 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali, kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.
“Napendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, kwa kupunguza tozo ya muamala kutoka kiwango kisichozidi shilingi 7,000 hadi kiwango kisichozidi shilingi 4,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa,” amesema Dk. Mwigulu na kuongeza:
“Punguzo hili ni sawa na asilimia 43 ya kiwango cha sasa. Sambamba na hilo, napendekeza kuongeza wigo wa tozo hiyo ili kuhusisha miamala yote ya kielektroniki. Lengo la hatua hii ni kupunguza makali ya maisha kwa mtanzania hasa katika kipindi hiki cha changamoto kubwa ya kiuchumi na kuweka usawa katika utozaji wa tozo hiyo.”
Leave a comment