July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali kupunguza mrabaha kwenye dhahabu, makaa ya mawe

Madini ya dhahabu

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, inakusudia kupunguza viwango vya mrabaha wa madini ya dhahabu na makaa ya mawe, yanayozalishwa nchini, katika mwaka wa fedha wa 2022/23. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumanne, tarehe 14 Juni 2022, bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2022/23.

Dk. Nchemba amesema, wizara yake inapendekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Madini, ili kupunguza kiwango cha kutoza marabaha kutoka asilimia sita hadi nne, kwa dhahabu inayouzwa kwenye vituo vya kusafisha madini.

“Lengo la hatua hii ni kuhakikisha kuwa vituo vilivyoanzishwa nchini vinapata malighafi ya kutosha kwa ajili ya kusafisha na hatimaye kuongeza ajira na mapato ya Serikali,” amesema Dk. Mwigulu.

Katika hatua nyingine, Dk. Mwigulu amesema, Serikali inakusudia kupunguza kiwango cha marabaha kutoka kwenye makaa ya mawe yanayotumika kama malighafi za kuzalisha nishati viwandani, kutoka asilimia tatu hadi moja.

“Lengo la hatua hii ni kupunguza gharama za uzalishaji viwandani, kuchochea uwekezaji zaidi na kukuza ajira,” amesema Dk. Mwigulu.

error: Content is protected !!