July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Watumishi hakuna kuhama na kiwango cha mshahara

Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama

Spread the love

 

SERIKALI imesema inakusudia kuondoa utaratibu wa Watumishi wa Serikali kuhama na mishahara yao pale wanapotoka kwenye nafasi za uteuzi au kuhamishwa ofisi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa leo Jumanne tarehe 14, Juni 2022, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/23.

Amesema imekuwa ni mazoea tangu uhuru viongozi wa nafasi za uteuzi na wakuu wa idara kuwama na kiwango cha mshahara wake hata uteuzi wake unapotenguliwa.

“Kwa mfano Makatibu Wakuu, Manaibu, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Makatibu Tawala wa Wilaya, wakurugenzi, wakuu wa taasisi mbalimbali, wakuu wa idara mbalimbali tangu uhuru wakitenguliwa huendelea kulipwa mshahara ule ule sawa na aliyeko kazini mpaka anastafu,” amesema Nchemba.

Amesema kutokana na hali hiyo unaweza kukuta nchi ina Wizara 25 ila ina Makatibu Wakuu 50 au zaidi, au Halmashauri 184 lakini kuna wakurugenzi 300 au zaidi na hivyo hivyo kwa nafasi nyingine.

“Wengine wamesababisha upotevu na hasara kwa Taifa, wote wanaendelea kuwabebesha mzigo watanzania na wanaziba nafasi ya ajira mpya kwa vijana kwa kulipwa mshahara wa nafasi walizotolewa.

“Napendekeza yeyote aliyetokea kwenye nafasi yake ya kuteuliwa akitolewa akabaki kwenye utumishi wa umma arejee pia kwenye mshahara wake wa zamani ili kuwapunguzia watanzania mzigo wa kuwalipa watu waliokaa benchi huku wakiziba nafasi za vijana wapya kuajiriwa,” amesema Dk. Mwigulu.

“Mambo haya hayavutii lakini lazima tuambizane ukweli. Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anakerwa kuona fedha nyingi zinakwenda kwenye matumizi ya kawaida,” amesema.

error: Content is protected !!