July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bei nywele bandia kutoka nje kupanda

Nywele bandia (mawigi)

Spread the love

 

BEI za nywele bandia maarufu kama mawigi, zinatarajiwa kupanda ifikapo Julai Mosi mwaka huu, baada ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuongeza ushuru wa forodha wa bidhaa hizo, kutoka asilimia 25 hadi 35. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ongezeko hilo limetolewa leo Jumanne, tarehe 14 Juni 2022 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2022/23.

Waziri huyo wa fedha amesema, lengo la ushuru huo kuongezwa ni kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo.

“Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa Heading 6704. Hatua hii inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na kuongeza mapato ya Serikali,” amesema Dk. Mwigulu.

error: Content is protected !!