Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Tangulizi TANAPA kutumia teknolojia kuimarisha ulinzi, usimamizi wa hifadhi
Tangulizi

TANAPA kutumia teknolojia kuimarisha ulinzi, usimamizi wa hifadhi

Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dk. Pindi Chana
Spread the love

 

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linatarajia kuimarisha ulinzi na usimamizi wa hifadhi kwa kuboresha matumizi ya sayansi na teknolojia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mali Asili na Utalii, Dk. Pindi Chana, leo Ijumaa tarehe 3 Juni, 2022, akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi yam waka 2022/23 bungeni jijini Dodoma.

Dk. Chana amesema TANAPA itanunua vifaa 20 vya mawasiliano ya mtandao mpana (LoRa Transmitters), ndege tatu (3) zisizo na rubani na kuweka mfumo wa redio za kidijitali katika vituo vitano katika Kanda ya Magharibi; na hifadhi za Taifa za Nyerere, Ruaha, Udzungwa na Mikumi.

Aidha amesema, Shirika litanunua vitendea kazi mbalimbali ili kuwezesha operesheni za doria kufanyika kwa tija na ufanisi zaidi.

Mbali namatumizi ya sayansi na teknolojia Chana amesema Shirika litaendelea kushirikisha jamii zinazoishi jirani na hifadhi katika shughuli za uhifadhi kwa kuimarisha vikundi 28 vya ulinzi shirikishi, vikundi 12 vya COCOBA na vikundi vitatu vya klabu za mazingira.

Vilevile, amesema elimu ya uhifadhi itaendelea kutolewa katika vijiji 864 vinavyozunguka hifadhi zote za Taifa na kuwezesha vijiji 11 kunufaika na miradi 11 ya ujirani mwema.

Mbali na hayo amesema, Shirika litawezesha ununuzi wa mizinga ya nyuki 800 kwa vikundi 24 vya jamii katika vijiji 24.

Katika hatua nyingine, Dk. Chana amesema Shirika litaendelea kudhibiti majanga ya moto kwenye hifadhi kwa kutengeneza mipango sita (6) ya usimamizi wa moto kichaa katika hifadhi za Taifa Nyerere, Kigosi, Mto Ugalla, Burigi – Chato, banda – Kyerwa na Rumanyika – Karagwe.

Sambamba na hilo, amesema Shirika litatekeleza Mipango ya Usimamizi wa Moto na kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi jirani na hifadhi kwa ajili ya kukabiliana na moto kichaa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!