Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yatoa siku 30 vigogo maliasili na utalii
Habari za Siasa

CCM yatoa siku 30 vigogo maliasili na utalii

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Balozi Pindi Chana
Spread the love

 

WIZARA ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania imepewa mwezi mmoja (siku 30) ihakikishe watendaji wake wa wanaohusika na wanyamapori wawe wamefika Meatu kutatua kero ya uvamizi wa tembo wanaoleta madhara katika makazi ya watu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Meatu … (endelea).

Aidha, watendaji hao wameambiwa kama hawawezi kutekeleza maagizo ya viongozi wa serikali na majukumu yao wakae pembeni ili wenye uwezo wafanye kazi hiyo kwani kuendelea kutotekeleza maagizo hayo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan tangu Februari 2022 ni dharau kubwa.

Wizara hiyo inaongozwa na Waziri Balozi Pindi Chana, Naibu wake ni Mary Masanja huku Katibu Mkuu ni Dk. Francis Michale na Naibu Katibu Mkuu ni Juma Mkomi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Jumatano tarehe 1 Juni 2022, wilayani Meatu mkoani Simiyu katika Kata ya Mwandu Itinje na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo alipokwenda kukagua uhai wa chama hicho na kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kupitia ilani ya chama hicho.

Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo katika moja ya ziara zake

Akisoma taarifa ya uhai wa chama hicho, Katibu wa Shina namba moja wa chama hicho katika kata hiyo ya Mwandu Itinje, Madeni Seni alisema kero kubwa mojawapo eneo hilo na kata nyingine ni uvamizi wa tembo wanaotoka pori la akiba la Maswa na hifadhi jirani wanaoleta uharibifu wa mazao na uhai wa binadamu.

Akijibu hoja hiyo, Chongolo alisema kero hiyo ni lazima ipatiwe ufumbuzi kwa sababu tarehe 4 Februari 2022, Rais Samia akiwa eneo la Lamadi njiani kuelekea Mara wananchi walitoa kilio hicho cha uvamizi wa tembo kwenye maeneo yao na kuomba serikali iingilie kuwadhibiti.

“Ni muda sasa umepita tangu Rais atoe maagizo kwa watendaji wa wizara ya maliasili kutekeleza hili la udhibiti wa tembo lakini hapa mmerudia tena kuwa hakuna hatua zilizochukuliwa,” alisema

“Hatuwezi kuwa na watu wanaoagizaa ila hawachukui hatua, hii ni dharau kwa kiongozi aliyekuagiza,sasa nakwenda ndani ya wiki nne (mwezi mmoja)wizara ya maliasili waje hapa waseme wamechukua hatua gani,” alisema Chongolo.

Alisema wananchi wamekuwa waungwana kutochukua hatua dhidi ya tembo licha ya wanyama hao kuharibu mazao na uhai wa wananchi na mnachotaka ni mamlaka iwadhibiti lakini watendaji husika wanaleta masihara kwenye mambo ya msingi.

“Mtu unapopewa dhamana lazima mkitumikie kwa wananchi na sio wawe na vilio visivyofika mwisho, yaani jana, leo na kesho ni kilio kile kile, siko tayari kuona vilio hivi visivyoisha,” alisema Chongolo.

Awali akizungumzia kero hiyo, Mwenyekiti wa CCM mkoani Simiyu, Shamsa Mohamed alisema kero hiyo imezungumzwa na kufikishwa kwa mamlaka husika lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hali inayowaumiza wananchi hao na maeneo mengine yanayoathiriwa na tembo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!