Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia akemea magari ya Serikali kubeba mikaa, ‘sombasomba’
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia akemea magari ya Serikali kubeba mikaa, ‘sombasomba’

Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi wa Uratibu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bi. Siajabu Pandu mfano wa funguo kama ishara ya kukabidhi gari kwa ajili ya utekelezaji kwa shughuli
Spread the love

 

RAIS Samia ameuagiza Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kushirikiana na TAMISEMI kuhakikisha magari 123 yaliyogawiwa kwa mfuko huo na Halmashauri, hayatumiki kwenda kubeba magunia ya mikaa au abiria ambao ni mtindo maarufu uliopewa jina la ‘sombasomba’. Anaripoti Erasto Masalu, Dar es Salaam … (endele).

Pia amewaagiza wafanyakazi wa TASAF kutumia fedha Sh trilioni mbili kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya kuwaachia walafi au midomo wazi kutafuna fedha hizo ambazo serikali imekopa kwa lengo la kuinua kaya maskini nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 1 Juni, 2022 jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ugawaji wa magari 123 kati ya 241 yaliyonunuliwa na Serikali na kugawiwa kwa TASAF pamoja na Halmashauri 184.

Ameagiza wakurugenzi wa halmashauri hizo kusimamia magari hayo yatumike kwa kazi iliyokusudiwa.

“Magari haya yasiende kubeba magunia ya mikaa na kuni, mbaya zaidi magari haya yanakwenda kubeba abiria nyakati za jioni wakati dereva anatoka sehemu moja kwenda nyingine anafanya ‘sombasomba’,” amesema Rais Samia.

Aidha, ametoa maagizo matano kwa TASAF ili magari hayo yatumike kwa ufanisi ambapo pamoja na mambo mengine ameagiza magari hayo kufungwa mfumo maalumu wa ufuatiliali ‘car trucking’ ili kuangalia matumizi na usalama wake.

Pili ni kuhakikisha magari hayo yanatumika kwa shughuli za TASAF mijini na vijijini, kama zilivyoainishwa katika mkataba.

“Utunzaji wa magari haya ni jukumu la halmashauri, magari haya yasiharibiwe kwa makusudi, kuna muda tutaangalia kuharibika kwake.

“Nne – Service ya magari haya ifanywe na wazoefu kwa maana Toyota ambao ndio watengenezaji wake, kwa kuwa wametuuzia kwa nusu bei, mkaongee nao watafanya kwa bei nafuu.

“Tano – magari ya zamani ambayo yalitolewa taarifa kuwa ni mabovu, yote yarudishwe ofisi za TASAF yakiwa na vifaa vyake,” amesema.

Aidha, ameiagiza TASAF kuhakikisha viongozi wa vyama vya siasa ambao wanakidhi vigezo vya kupatiwa ruzuki, wapewe fedha hizo ili waweze kujikwamua katika lindi la umaskini.

Amesema TASAF imekuwa taswira halisi ya serikali inayojali watu wake na kuwafikia wananchi wenye uhitaji katika vijiji, mitaa na shehia zote Tanzania bara na Zanzibar lengo ni kuwatoa katika lindi la umaskini.

“Lengo la jumla la serikali kuanzisha TASAF lilikuwa ni kupunguza umasikini na kwa hivyo serikali tunafarijika sana kusikia na kuona kwamba lengo hilo linaendelea linafikiwa.

“Taarifa zinasema hadi kufikia mwaka huu -2022, TASAF imeonesha mpango huu umechangia kupunguza umaskini wa mahitaji ya msingi ya kaya kwa zaidi ya asilimia 10 na umaskini uliokithiri kwa zaidi ya asilimia 12,” amesema Rais Samia.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga amesema katika awamu ya tatu kipindi cha pili cha mpango huo wa TASAF, wameandikisha kaya 498,091.

“Mambo mengi yamefanyika ambayo ni uhakiki wa awali wa kaya ambao umefanyika katika mamlaka zote 186 za utekelezaji ambapo jumla ya kaya 886,724 zilihakikiwa na kaya 781,342 zilikidhi vigezo vya uhakiki wa awali na kuendelea na mpango,” amesema.

1 Comment

  • Kumbe fedha za TASAF ni za kukopa? Tuone mkataba na masharti na jinsi tutakavyolipa. Ni uwekezaji wa ajabu huu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!