Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Vipaumbele 12 vya Makamba Wizara ya Nishati
Habari za Siasa

Vipaumbele 12 vya Makamba Wizara ya Nishati

January Makamba, Waziri wa Nishati
Spread the love

 

WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba amekuja na vipaumbele 12 katika utekelezaji wa bajeti ya mwkaa 2022/23. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Leo Jumatano tarehe 1 Juni, 2022, Makamba amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake ya jumlaya Sh 2.7 trilioni.

Katika hotuba yake amebainisha kuwa katika kutekeleza Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2022/23, Wizara Wizara itaongozwa na vipaumbele 12 ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme.

Makamba amesema usambazaji umeme utahusisha kupeleka umeme wa Gridi ya Taifa kwenye mikoa ya Katavi, Kigoma na Kagera na mradi mkubwa wa Kuimarisha Gridi ya Taifa.

Kipaumbele kingine ni kutekeleza Miradi ya Nishati Vijijini pamoja na kuanza utaratibu wa kupeleka umeme katika Vitongoji vyote nchini.

Vingine ni kukamilisha mazungumzo ya mradi wa LNG Lindi na kuanza maandalizi ya utekelezaji wake; kutekeleza miradi ya nishati jadidifu ikiwemo jotoardhi, tungamotaka, upepo na jua pamoja na matumizi bora ya Nishati.

Makamba ametaja vuipaumbele vingine kuwa kuhakikisha upatikanaji wa mafuta ya kutosha nchini, kuiimarisha TPDC na Kampuni zake Tanzu za TANOIL na GASCO; kuboresha miundombinu ya kupokea, kushusha, kuhifadhi na kutoa mafuta katika Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na Ghala za dhamana ya forodha na Kituo cha Pamoja cha kupokelea Mafuta kutoka Melini.

Vingine ni kuimarisha utendaji wa taasisi za Wizara, hasa TANESCO, EWURA na PBPA, na huduma zinazotelewa na taasisi hizo; kuongeza ushiriki na uwekezaji wa Sekta Binafsi katika sekta ya Nishati; kuhakikisha ushiriki wa wazawa katika shughuli za mafuta na gesi asilia unaimarika; kufufua Shughuli za utafiti na utafutaji wa mafuta na gesi asilia na kuongeza matumizi ya nishati ya gesi kwa kupikia (LPG) na kwenye magari na viwandani (CNG).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Jaji Biswalo aendelea kung’ang’aniwa fedha za ‘Plea Bargaining’, CUF wataka ajiuzulu

Spread the love  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimemtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka...

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

error: Content is protected !!