Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe azungumzia Rais Samia kutinga uzinduzi kitabu cha Sugu
Habari za Siasa

Mbowe azungumzia Rais Samia kutinga uzinduzi kitabu cha Sugu

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Chadema, Freeman Mboiwe, amesema hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan, kuzindua kitabu cha msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop Tanzania, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu, ni sehemu ya safari ya nchi katika kufikia mshikamano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe ametoa kauli hiyo jana Jumanne, tarehe 31 Mei 2022, katika uzinduzi wa kitabu hicho chenye jina la Muziki na Maisha from the street, uliofanyika kwenye tamasha la Dream Concert, Serena Hotel, jijini Dar es Salaam.

“Siwezi kusema ni mwanzo mzuri kwa sababu tayari tumeshakutana na tutaendelea kukutana na kutoa taarifa hatua kwa hatua kwa namna ambavyo tunaendelea kukutana. Lakini ni sehemu ya safari na tumeonesha kwamba we are serious katika hili,” amesema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa Chadema, amewaomba Watanzania wamalize tofauti zao na kuijenga Tanzania.

“Ni matumaini yangu kwamba Watanzania wote wenye kupenda mshikamano katika taifa letu, wataona umuhimu wa kumaliza tofauti zetu na kuijenga Tanzania iliyokuwa na ushirikiano bora zaidi,” amesema Mbowe.

Tangu alivyoingia madarakani Machi 2021, kufuatia kifo cha mtangulizi wake, aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magifuli, Rais Samia amekuwa na desturi ya kutafuta maridhiano na makundi mbalimbali, ikiwemo vyama siasa na viongozi wa dini.

Rais Samia ameshafanya mazungumzo na Mbowe mara mbili, Ikulu ya Dar es Salaam, pamoja na viongozi wa Chadema, Chama cha Wananchi (CUF) na ACT-Wazalendo.

Katika kutafuta maridhiano, Rais Samia ameunda kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kukusanya maoni ya wadau kwa ajili ya kuboresha demokrasia ya vyama vingi vya siasa, ikiwemo marekebisho ya katiba, tume za uchaguzi na shughuli za kisiasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!