Tuesday , 30 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bashungwa aagiza nafasi za kukaimu zijazwe
Habari Mchanganyiko

Bashungwa aagiza nafasi za kukaimu zijazwe

Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amewaelekeza Katibu Mkuu, Utumishi na TAMISEMI kufanya maamuzi katika nafasi wanazokaimu Maofisa Utumishi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Waziri Bashungwa ameyasema hayo Jijini Dodoma tarehe 27 Mei, 2022 wakati akifunga kikao kazi cha Wakuu wa Idara/Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma lengo likiwa kuwakumbushwa wajibu wao katika uwajibikaji kazini, uadilifu na ubunifu katika kazi.

Amesema bado kuna Maofisa Utumishi ambao wamekaimu nafasi hizo kwa muda mrefu na kwamba kama wanasifa zinazohitajika ni vyema kuthibitishwa ili kuongeza ufanisi kwenye majukumu yao.

“Nafasi za kukaimu kwa muda mrefu zinavyoweza kusababisha uzorotoshaji wa kazi kwa kutoheshimiana, kudharauliana hata kusababisha kutokutoa huduma bora kwa wananchi,” amesema.

Kutokana na hali hiyo, Waziri Bashungwa amemuelekeza Katibu Mkuu, Utumishi Dk. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu, TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kulifanyia maamuzi ya haraka kwa maafisa waliokaimu kwa muda mrefu wa Sekretariet za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma ili kama wanasifa ya uteuzi kwa nafasi husika.

“Mtumishi mwenye uteuzi wa nafasi yake moja kwa moja ni dhahiri tutaongeza uwajibikaji, heshima na ufanisi katika kazi” amesema Bashungwa.

Aidha, amewaelekeza baadhi ya maafisa utumishi kuacha kutoa lugha zisizo kua na ari kwa watumishi wenzao kufanya kazi amesema, usimamizi wa rasilimaliwatu unaendana na uzalishaji wa uchumi wa nchi na hii inaendana na shabaha ya Serikali katika kutoa huduma bora kwa wananchi.

“Kila mtumishi anawajibu wa kusikilizwa sababu kila mmoja anamchango wake kwa Taifa tushirikiane katika kuhakikisha tunafanya kazi Kwa kufuata taratibu za kazi.

“Pia Serikali ya Samia Suluhu Hassan imeaminika kwa ajili ya kusimamia wananchi na Serikali hii ndio inayotekeleza Ilani ya chama kwa kuhakikisha inatoa huduma bora kwa waliotuamini ambao ni wananchi wenzetu” amesema Bashungwa

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

7 wafa Ulanga, mbunge alia kutelekezwa na mawaziri, Tanroad

Spread the loveWatoto saba wamepoteza maisha na zaidi ya kaya 70 kukosa...

Habari Mchanganyiko

Bil 12.4 zimetumika ujenzi wa miradi wilaya ya Momba

Spread the love MKUU wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi...

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

error: Content is protected !!