Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bosi NMB ashinda tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji Bora wa Kibenki Afrika 2022
Habari Mchanganyiko

Bosi NMB ashinda tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji Bora wa Kibenki Afrika 2022

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna
Spread the love

AFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna ametangazwa kuwa mshindi wa kipengele cha Afisa Mtendaji Mkuu Bora Africa kwa Mwaka 2022 (Tanzania). Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Ni katika kipengele cha Benki na Uongozi wakati wa hafla iliyofanyika Ijumaa ya tarehe 27 Mei 2022 Koteli Movenpick jijini Nairobi nchini Kenya.

Tuzo hiyo ilitolewa na Julias Alego Mkurugenzi Mtendaji Tasisi ya Mabenki nchini Kenya na kupokelewa na Mweka Hazina Mkuu wa Benki ya NMB, Aziz Chacha.

Chacha, akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna alisema,”ni heshima kubwa sana kuwa nanyi usiku wa leo kupokea Tuzo ya “African Banking CEO of the Year 2022 (Tanzania)” kwa niaba ya Ruth Zaipuna, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mabenki Kenya Julius Alengo akimkabidhi tuzo Mweka Hazina wa benki ya NMB Aziz Chacha ambaye alipokea tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu Bora Afrika kwa Mwaka 2022 (Tanzania) kwa niaba ya Ruth Zaipuna ambaye hakuwepo, katika afla iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Nairobi.

Mara baada ya kupokea Tuzo hiyo kwa niaba ya Ruth wa NMB, Chacha alisema Ruth ameitoa tuzo hiyo kwa wafanyakazi wa NMB kwa kujitolea kwao na nia ya kuendelea kuwa mstari wa mbele wa vumbuzi, kuzingatia wateja, uthabiti, uaminifu, na usalama.

“Kwa maneno ya Ruth, natoa tuzo hii maalum kwa moja ya mtaji wetu mkubwa ambao ni wafanyakazi wa benki ya NMB ambao bila wao, pengine tusingekuwa hapa tulisherehekea,” amesema

Amebainisha benki yake kwa miaka mingi imekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia shughuli mbalimbali za kiuchumi katika sekta nyingi ikiwemo utalii, elimu, kilimo, miradi ya kimkakati ya muda mrefu na afya.

“Ninatoa tuzo hii kwa wadau wa benki  ya NMB ambao wamejitolea kikamilifu katika azma yetu ya kubaki kweli bila kulinganishwa – benki imekuwa mstari wa mbele kwenye suala zima la ubunifu kwa kuzingatia wateja, uthabiti, uaminifu, usalama na usalama,” amesema.

Machi 2022, Ruth alitajwa kuwa miongoni mwa wanawake 74 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika katika sherehe za wanawake wanaofanya biashara kubwa barani Afrika na data zilizotumika kutengeneza orodha hiyo ilitolewa kutoka Bloomberg kulingana na taarifa iliyotolewa na Africa.com.

Orodha hiyo iliwakilisha wanawake wanaofanya biashara kubwa barani Afrika. Biashara zote zinazoendeshwa na wanawake zenye Mapato ya USD100 milioni au zaidi.

Viongozi wengine wanawake waliotajwaa ni pamoja Natascha Viljoen, Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Anglo American Platinum; Nompumelelo Thembekile Madisa, Afisa Mkuu Mtendaji wa Bidvest Group na Leila Fourie, Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Johannesburg.

Viongozi wengine wanawake wa Afrika Mashariki kwenye orodha hiyo ni pamoja na Mitwa Ng’ambi, Afisa Mtendaji Mkuu wa MTN Rwanda Telecommunications, Kendi Ntwiga-Nderitu, Mwakilishi wa kampuni ya Microsoft nchi, Kenya na Brenda Mbathi, nktugugenzi wa kampuni ya General East Africa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!