Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yatenga bilioni 1 kusaidia wabunifu wachanga, Waziri apongeza
Habari Mchanganyiko

NMB yatenga bilioni 1 kusaidia wabunifu wachanga, Waziri apongeza

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Juma Kipanga (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Meneja wa idara ya Ubunifu wa benki ya NMB, Proches Kachenje (katikati) alipotembelea Banda la NMB wakati anazindua wiki ya Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto ni meneja wa Benki ya NMB tawi la Chuo Kikuu, Kingsley Chilambo. Benki ya NMB imedhamini maonesho hayo yaliyoanza Jumanne ya tarehe 24 mwezi huu na yatamalizika Alhamisi ya tarehe 26.
Spread the love

BENKI ya NMB nchini Tanzania imetenga kiasi Sh.1 bilioni kwa ajili ya kuwasaidia wabunifu wachanga waweze kuimarika na kuzifanya bunifu zao kuwa bora na zenye manufaa kwao na kwa uchumi wa Taifa kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 24 Mei 2022 na Meneja Idara ya Ubunifu kutoka Benki ya NMB, Proches Kachenje alipokuwa anamuelezea Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga alipotembelea banda la NMB wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Naibu waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Juma Kipanga (wa pili kulia) akisalimiana na maafisa wa Benki ya NMB alipotembelea Banda la NMB wakati anazindua wiki ya ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ubungo, Heri James. Benki ya NMB imeshiriki na Kudhamini maonesho hayo yaliyoanza Jumanne ya tarehe 24 mwezi huu na yatamalizika Alhamisi ya tarehe 26.

“NMB imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja kwaajili ya kuwasaidia wabunifu wanaochipukia kuweza kuziweka bunifu zao katika utekelezaji ili ziweze kutekelezeka na hatimae ziwanufaishe wabunifu hao,” amesema Proches.

Amesema mbali na kuwepo kwa mfumo wa kutoa fursa za majaribio kwa wabunifu hasa wa masuluhisho ya kifedha, bado NMB imeona ipo haja ya kutenga na fedha kwaajili ya kuwawezesha wabunifu waweze kuziweka katika utekelezaji bunifu zao.

“Mwaka jana tulizindua mfumo maalumu tuyliouita NMB sandbox environment ambapo wabunifu wa suluhishi mbalimbali za kifedha wanaweza kufanya majaribio ya bunifu zao na kwa zitakazo fuzu kuendelezwa kwa ushirikiano wa wabunifu hao na benki ya NMB, lakini kwa kutambua Changamoto haswa za kifedha wanazopitia wabunifu, tumeona ni vyema tukatenga na kiasi hiki cha fedha kuwasaidia,” amesema

Proches amesema kiasi hicho cha fedha sio mkopo bali ni fedha iliyotengwa kwa dhumuni ya kusaidia wabunifu hawa na hawatawajibika kuirejesha. Alitumia pia fursa hiyo kuwakaribisha wanachuo na Vijana wabunifu kuishirikisha Benki ya NMB juu ya bunifu zao kwani kwa kufanya hivyo inweza kuwasaidia kupata fedha za kuboresha zaidi.

 

Aidha, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Kipanga amewapongeza Benki ya NMB kwa kuwajali wabunifu na kuwasihi washirikiane vyema na wizara ya elimu ili waweze kuwafikia wabunifu wengi zaidi.

“Wazo hili ni zuri sa na niwapongeza kwa hilo. Tukishirikiana vyema tunaweza kuwafikia wabunifu wengi sana, na kwa kufanya hivyo mnakwenda kusaidi kupunguza changamoto ya Ajira,” alisema Kipanga.

Benki ya NMB imeshiriki na kudhamini maonesho ya ubunifu ya Chou Kikuu cha Dar es Salaam ambayo yameanza leo Jumanne na yatamalizika Alhamisi tarehe 26 Mei 2022 yakiwa na lengo ya kuonesha bunifu mbalimbali kutoka chuo hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!