HADI kufikia tarehe 30 Aprili, 2022 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (Fungu 68) imepokea jumla ya Sh. bilioni 129.7 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambayo ni asilimia 53.7 ya fedha zilizotengwa. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa tarehe 20 Mei 2022 na Waziri wa Habari, Nape Nnauye, akiwasilisha makadiirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.
Katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliidhinishiwa kutumia kiasi cha Sh. 246.3 bilioni.
Nape amesema kati ya fedha hizo Sh. 4.9 bilioni iliidhinishwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Sh. 241.3 iliidhinishwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Aidha, ameongeza kuwa Idara ya Habari – MAELEZO na Taasisi za TBC na TSN zilikuwa zimetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi 23.7 bilioni kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali.
Amesema kati ya fedha hizo Sh. 17.7 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya awaida na Sh. 6 bilioni ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Kwa upande wa bajeti ya Matumizi ya Kawaida Nape amesema hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2022 Wizara imepokea na kutumia jumla ya Sh. 6.9 bilioni sawa na asilimia 84 ya fedha zilizotengwa.
Amesema kati ya fedha za matumizi ya kawaida zilizopokelewa Sh. 2.2 bilioni ni za Mishahara na Sh. 4.6 bilioni ni Matumizi Mengineyo.
Leave a comment