Tuesday , 7 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbowe atoa kauli kina Mdee kubaki bungeni
Habari za SiasaTangulizi

Mbowe atoa kauli kina Mdee kubaki bungeni

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe ameonesha kushangazwa na uamuzi wa Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kuwabakiza bungeni Halima Mdee na wenzake 18 licha ya kufukuzwa ndani ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mdee na wenzake walifukuzwa Chadema tarehe 27 Novemba 2020 na kamati kuu ya chama hicho wakituhumiwa kughushi nyaraka za chama, usaliti na kisha kujipeleka bungeni jijini Dodoma kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum.

Baada ya kufukuzwa, walikata rufaa Baraza Kuu la chama hicho lililokutana tarehe 11 Mei 2022 jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kuzisikilizwa wajumbe 413 kati ya 423 zilikubaliana na kilichofanywa na kamati kuu ya kuwafukuza.

Hata hivyo, kabla ya uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kutoa zuio la Mdee na wenzake 18 kuondolewa Bungeni jioni jana Jumatatu, tayari Spika Tulia asubuhi yake alikuwa amekwisha kueleza hatowaondoa bungeni kwani kuna kesi mahakamani.

Mahakama Kuu chini ya Jaji John Mgeta ilitoa zuio hilo hadi tarehe 13 Juni 2022 itakapoanza kusikiliza kesi ya msingi pamoja na kupokea nyaraka mbalimbali zinazohusu kesi hiyo.

MwanaHALISI Online lilizungumza na Mbowe baada ya uamuzi wa Spika Tulia akisema, “sisi tumemaliza kazi yetu, wacha wagombane na wananchi kwani hakuna kilicho sawa, kama Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameamua kuwalinda kwa mgongo huo sawa.”

Mbowe alihoji, “hivi Mahakama inaingiliaje shughuli za Bunge ama Bunge linaingiliaje shughuli za Mahakama ikiwa mihimili hii inajitegemea? Tutasubiri na tutaona mbele ya safari.”

Wakili Jebra Kambole katika ukurasa wake wa Twitter aliandika, “kama mahakama imetoa zuio (injunction) la mchakato wa kibunge sawa!, Lakini kama ni barua tu ya kutoka upande mmoja basi spika na Bunge lake wanageuka kihoja waozuiliwa kutenda jambo kwa barua badala ya amri! Mahakama haitoi barua inatoa orders tu! Bila stop order ni usanii hapo!”

Kambole anaungana na Wakili Fredrick Kihwelo akisema, “Spika amejielekeza vibaya, hakuna amri au zuio la Mahakama juu ya kushughulikia suala la Halima na wenzake 18.”

“Kwa maelezo yake amefanya uamuzi huo kwa misingi ya barua ya Mdee na wenzake na shauri lilipo Mahakamani. Uwepo wa shauri mahakamani haujawahi kuwa zuio,” alisema Kihwelo na kuongeza:

“Mara kadhaa Bunge hili limetoa maamuzi kwamba ni mhimili unaojitegemea kwahiyo hauwezi kuingiliwa na Mahakama au mhimili mwingine. Leo mhimili huo umeingiliwa na barua za Halima na wenzake 18.”

1 Comment

  • Kwa Tanzania hii tutazidi kuona vioja vingi sana sijui Kuna nini hapo ccm inapotumia nguvu namna hii kuwalinda COVID 19

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!