Tuesday , 19 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama yawapa nafuu ya wiki Mdee na wenzake
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama yawapa nafuu ya wiki Mdee na wenzake

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imesema wabunge 19 wa Chadema (Covid 19) waliovuliwa uanachama wa chama hicho hivi karibuni wataendelea kuwa wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano Tanzania mpaka pale Mahakama itakaposikiliza maonbi yao ya zuio la muda Juni 13, 2022. Anaripoti Fakhi Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Uamuzi huo umetolewa na Jaji John Mgeta leo Mei 16, 2022 wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Maombi hayo namba 13 ya mwaka 2022 ni maombi madogo kwenye shauri la msingi namba 16 la mwaka 2022 ambapo wabunge hao wanaomba mahakamani hapo kurejeshewa uanachama wao.

Uamuzi wa kuvuliwa uanachama kwa wabunge hao ulihitimishwa wiki iliyopita baada ya Bazara Kuu la Chadema kukubaliana na uamuzi wa Kamati Kuu dhidi ya rufaa za wanachama hao.

Maombi hayo yamefunguliwa dhidi ya bodi ya wadhamini ya Chadema, Tume ya Taifa ya uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mdee na wenzake wamefungua maombi ya zuio la muda ( injunction) wanaomba waendelee kuwa wabunge hadi uamuzi wa maombi yao ya msingi yatakapotolewa.

Awali mahakamani hapo Wakili Peter Kibatala, Jeremiah Mtobyesya mawakili walioiwakilisha Chadema wamewasilisha mahakamani hapo hoja sita za kupinga kukubaliwa kwa zuio hilo mahakamani hapo ambazo zilijikita kwenye madai ya kasoro zilizopo kwenye hati ya kiapo cha waombaji.

Kibatala amedai Mahakamani hapo kiapo kina dosari ya kutotanabaishwa dini za waapaji (Mdee na wenzake), “Viapo vyao mahitaji dini zao ikitokea wanataka kuapa wataapa kwa kitabu gani?”.

Hoja nyingine Kibatala amedai Mahakamani hapo waombaji wameomba waendelee na nyadhifa zao bila kueleza hoja hiyo zinakwenda kwa nani kama ameelekezwa Spika wa Bunge au Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

“Oda za Mahakama hunyooka zinatekelezeka”.
Kibatala amesema kuwa waombaji wameomba nafuu ya kuendelea kuwa wanachama wa Chadema bila kubainisha nafuu hiyo waipate kwa nani.

Hoja ya Mwisho Kibatala ameiomba Mahakama hiyo kutupilia mbali zuio hilo kwani kiapo hicho hakijakidhi sharti la zuio la kuwa wanaomba zuio juu ya hatari gani.

Upande wa waombaji amesisitiza mahakama kutoa amri ya zuio hilo kwa upande wa wajibu maombi hakuwa na hoja za kutosha kuzuia mahakama kutotoa zuio hilo kwa kuwa hawajaweka wazi sheria ipi inataka waapaji wateja dini zao.

Jaji Mgeta akitoa uamuzi huu amesema kuwa mahakama hiyo inazuia wabunge hao kuondolewa kwenye nyadhifa zao mpaka tarehe 13 Juni ambapo mahakama itasikiliza mashauri yote mawili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Zanzibar mbioni kuanza uchimbaji mafuta na gesi baharini

Spread the loveSERIKALI ya Zanzibar, imekamilisha mchakato wa uchimbaji wa mafuta na...

Habari za Siasa

Wizara ya afya yataja mafanikio 10 miaka mitatu Samia madarakani

Spread the loveWIZARA ya Afya imetaja mafanikio 10 iliyoyapata ndani ya miaka...

Habari za Siasa

Mbozi walilia kuwa manispaa, majimbo 3

Spread the loveHALMASHAURI ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe imeeleza dhamira yake...

Habari za Siasa

Wabunge waitaka TPDC kuongeza kasi ya kuunganisha wateja gesi asilia

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini...

error: Content is protected !!