Tuesday , 30 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM waitaka Serikali itoe ufumbuzi kupanda kwa bei ya mafuta
Habari za Siasa

CCM waitaka Serikali itoe ufumbuzi kupanda kwa bei ya mafuta

Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa namna ya kukabiliana hali ngumu ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta duniani ili kuwapunguzia wananchi makali ya maisha. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 9 Mei, 2022 na Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka imesema chama hicho kimetoa maagizo hayo kwa kuwa kimeguswa na hali hiyo ya maisha iliyopo nchini.

“Tunafanya hivyo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zetu kupitia ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ambayo tuliahidi kuisimamia serikali ili kuwaletea maendeleo Watanzania na kuimarisha ustawi wao.

“Pamoja na sababu za kitaalamu zinazotajwa kusababisha kupanda kwa bei ya mafuta na kupelekea mfumuko huu wa bei nchini, chama makini na serikali inayojali watu wake haiwezi kukaa kimya na kukosa hatua za kuchukua hatua ili kuwapunguzia mzigo wananchi,” amesema.

Amesema kutokana na hali hiyo CCM kimeitaka serikali kukaa na kuchukua hatua haraka ili kuwapa nafuu ya maisha wananchi.

Aidha, CCM kimewaomba Watanzania kuwa watulivu na kuendelea kuiamini serikali ya CCM ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati huu ambao inaendelea kuchukua hatua stahiki za kupunguza makali hayo bila kuathiri shughuli zingine za maendeleo ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

1 Comment

  • Ile Sera imesema nini juu ya kukabiliana na athari za nje ya nchi?
    Kwa nini Tanzania hatuna mkakati wa akiba ya Taifa?
    Hii pia ndiyo ingeipandisha nchi uchumi wa juu. Kwa nini CCM haikabiliani na rushwa kama Enzi zile za Baba wa Taifa. Haiwajibishi watu wenye tuhuma.
    Haipazi sauti Tume ya Maadili iwe na meno.
    Sasa tutaiambia nini serikali yetu wakati hatuoni haki ilitendeka kwa walioiba mabilioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

Habari za SiasaTangulizi

Samia ataja miradi ambayo Tanzania inashirikiana na IDA

Spread the loveRais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu amehutubia...

error: Content is protected !!