Sunday , 19 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Gavana Benki Kuu ajitosa urais
Kimataifa

Gavana Benki Kuu ajitosa urais

Gavana wa Benki Kuu ya Nigeria (CBN), Godwin Emefiele
Spread the love

 

GAVANA wa Benki Kuu ya Nigeria (CBN), Godwin Emefiele amejitosa katika kinyang’anyiro cha kuteuliwa na chama cha All Progressive Congress kuwa mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka kesho. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Msemaji wa chama hicho, Joseph Morka amewaeleza waandishi wa habari kuwa gavana huyo mwenye umri wa miaka 60, amechukua fomu kwa thamani ya zaidi ya Sh milioni 500 kuwania kumrithi Rais wa sasa Muhammadu Buhari ambaye anamaliza muda wake.

Gavana huyo amehudumu katika nafasi hiyo nyeti kwenye sekta ya fedha tangu mwaka 2014, baada ya kuteuliwa na Rais wa Nigeria wakati huo, Goodluck Jonathan kisha Buhari.

Kufuatia uamuzi huo, sasa Gavana huyo amekumbana na shinikizo la kutakiwa kujiuzulu kutokana na sheria za nchi hiyo kumtaka mtumishi yeyote wa serikali anayejiingiza katika kinyang’anyiro chochote cha kisiasa ndani ya siku 30 awe amejiuzulu nafasi yake.

Emefiele ameungana na Makamu wa Rais, Yemi Osibanjo, Gavana wa jimbo la Lagosi, Bola Tinubu na Waziri wa uchukuzi, Rotimi Amechi katika kuwania kuteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Bunge kumuweka katibu mkuu wa EAC kikaangoni

Spread the loveAliyekuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dk. Peter...

Kimataifa

Palestina mwanachama wa 194 wa UN

Spread the loveBaraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Ijumaa limepitisha kwa...

Habari za SiasaKimataifa

Israel yatia shubiri Gaza wakisherehekea Hamas kusitisha mapigano

Spread the loveWAKATI kundi la Hamas huko Gaza likitangaza kuridhia pendekezo lao...

KimataifaMakala & Uchambuzi

Mbivu, mbichi urais wa Ramaphosa mwezi huu

Spread the loveMWISHONI mwa mwezi huu, raia wa Afrika Kusini watapiga kura...

error: Content is protected !!